loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mgombea Chadema apigwa ‘stop’ siku 3

KAMATI ya Maadili ya Tume ya Uchaguzi Jimbo la Sumbawanga Mjini imemfungia mgombea ubunge katika jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Shadrack Malila asifanye kampeni kwa siku tatu kuanzia leo.

 

Kamati hiyo imesema imechukua hatua hiyo kutokana na mgombea huyo kutoa kauli za uchochezi na maudhi katika moja ya kampeni zake za uchaguzi.

Kwa mujibu wa kamati hiyo, leo Malila atakabidhiwa barua kumjulisha kuhusu uamuzi huo ili aanze kutumikia adhabu hiyo. Malila pia ni Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Rukwa.

Mgombea huo alisema mwakilishi wake aliyehudhuria kikao cha Kamati ya Maadili amempa taarifa kuhusu adhabu hiyo na kwamba ataipinga kwa madai kuwa ni batili.

 

"Nikikabidhiwa rasmi barua hiyo na kuisoma ndipo nitatoa maamuzi ya kuendelea na kampeni zangu au nitasitisha,” alisema.

Mgombea huyo ni mara ya pili kuwania ubunge katika jimbo hilo ambapo mara ya kwanza ilikuwa 2015 na kushindwa.

 

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu anachuana na Mbunge aliyemaliza muda wake Aish Hilaly (CCM), Doris Kafuku (NCCR-Magauezi), Julius Mizengo (CUF), Michael Lubava (UDP) na Suleiman Abdallah Sinani (ACT-Wazalendo)

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi