loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mhadhiri dini ya Kiislamu ataka watu kupinga vitendo vya uvunjifu wa amani

MHADHIRI maarufu wa dini ya kiislamu Shehe Nurdin Kishki amewataka Watanzania katika kipindi hiki cha kampeni za vyama vya siasa na kuelekea Uchaguzi Mkuu kuwapinga watu ambao kwa namna moja au nyingine wanafanya vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani.

Shehe Kishki ameyasema hayo katika hotuba yake ya Ibada ya swala ya Ijumaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika Msikiti wa Temeke Vetenari.

Alisema kuwa haki, usawa na uadilifu vikifuatwa katika mchakato mzima wa Uchaguzi Mkuu vitaivusha Tanzania salama.

Katika hotuba hiyo aliyoipa kichwa cha habari 'Mv Tanzania'alinukuu hadithi ya Mtume Muhammad(SAW) katika kitabu cha mpangilio wa hadithi iliyokuwa ikielezea kisa kisa cha watu wa jahazi.

Katika hadithi hiyo, Mtume Muhammad alitolea mfano wa watu ambao walikuwa wakisafiri ndani ya jahazi katika moja ya bahari kubwa lakini ndani ya hilo jahazi walikuwa wamekaa katika safu mbili ya juu na ya chini lakini mahitaji yote muhimu ndani ya hilo jahazi ikiwemo maji na chakula yapo katika watu wa safu ya juu, kila watu wa chini wakihitaji walikuwa wakiwaomba watu wa juu  ambao mwishowe wakawa wanaona kero hatimaye wakaja na wazo la kulitoboa jahazi ili maji yaingie wasiwasumbue watu wa juu.

"Ndugu zangu mimi si mwanasiasa, sihubiri siasa na wala sitahubiri siasa na haya ninayozungumza naomba unielewe kwa sikio lisilo la ushawishi wa kisiasa katika kipindi hiki cha kampeni na kuelekea Uchaguzi Mkuu, naomba tujiepushe na watu ambao wanaleta viashiria vya uvunjifu wa amani, tusiwe kama watu wa jahazi ambao wanataka kutoboa jahazi mwishowe watazama wote,"alisema na kuongeza:

"Mimi nimetembelea takribani nchi 13 duniani ikiwemo Rwanda ambaye ndiye kiongozi wa kwanza wa dini kutembelea jumba la Makumbusho la mafuvu ya watu waliokufa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994, hali inatisha Wanyarwanda kila wakiingia humo ndani wakitoka wanalia wanajua madhila ya ukosefu wa amani".

"Sasa wewe ambaye unataka kuvunja amani kwa ajili ya mgombea udiwani, ubunge, urais amani ikitoweka wenzako wanakimbilia nje ya nchi wewe huna hata 'passport' (hati ya kusafiria) utakimbilia wapi? Je, tutaswali kwa jamaa kama hivi? Au utaendesha bodaboda au utafanya ujasiriamali?".

foto
Mwandishi: Cheji Bakari

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi