loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wakerwa na ukandamizaji wanawake wanaogombea nafasi za siasa

VYAMA vya siasa hapa nchini vimetakiwa kuacha vitendo vya ukandamizaji, uonevu na udhalilishaji  kwa wanawake wanaogombea nafasi mbalimbali za uwakilishi ikiwemo ngazi ya ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu unatorajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Taasisi zisizokuwa za  kiserikali mkoani Mtwara zinazojishughulisha na masuala ya kijamii kwenye manispaa hiyo ikiwemo Door of Hope, Mtwangonet, Fawopa, Nerio zimetoa tamko hilo wakati wa kikao na waandishi wa habari kilichofanyika mjini Mtwara.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya utetezi, uwezeshwaji na usaidizi wa wanawake hapa nchini (Door of Hope), Clemence Mwombeki alisema wamekuwa wakiunga mkono serikali hasa kipindi hiki hususani mashirika ya wanawake na yanayotetea haki za  wanawake na yamekuwa yakiendelea kuhamasisha ushiriki wa wanawake kwenye ngazi mbalimbali za maamuzi.

Mratibu wa Mtwangonet mkoani humo, Fidea Ruanda alisema wameona idadi kubwa ya wanawake wamejitokeza kupitia vyama vyao mbalimbali vya siasa hata kama idadi ya wanawake hao haijawa kubwa ikilinganishwa na wanaume lakini jitihada zao zimesaidia kuwepo kwa ongezeko hilo.

Baadhi ya wagombea wa nafasi hizo za uongozi akiwemo mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Mtwara mjini, Tunza Malapo alikiri kuwepo kwa vitendo hivyo vya udhalilishaji wanawake na kutoa mfano kuchaniwa mabango yao ya uchaguzi na lugha zisizokuwa nzuri kwao ilihali tu kumkatisha tamaa mwanamke ili asigombee .

Mgombea udiwani wa Kata ya Mtonya kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Mtwara Mjini, Shadida Ndile amekiri kuwepo kwa lugha hizo za kumdhalilisha mwanamke zinazotolewa na baadhi ya wagombea wa vyama hivyo vya siasa jambo ambalo alieleza kuwa sio zuri. 

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Mtwara

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi