loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

CCM yatamba kulisomba jimbo la Segerea

CHAMA cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kimesema uchaguzi wa Oktoba 28 mwaka huu kitashinda kwa kishindo nafasi zake zote za ubunge, udiwani pamoja na nafasi ya urais.

Mgombea udiwani wa CCM Kata ya Kiwalani, Mussa Kafana ambaye awali alikuwa Chama cha Wananchi(CUF), alisema hayo kwenye mkutano wa kampeni wa Jimbo la Segerea Kata ya Minazi Mirefu wakati akimwombea kura mbunge Bonah Kamoli, diwani wa Kata ya Minazi Mirefu Godlisten  Malisa pamoja na mgombea urais John Magufuli.

Kafana alisema katika Jimbo la Segerea wakati akiwa CUF alichangia CCM ikose madiwani katika Jimbo la Segerea hivyo kwa sasa amerudi CCM  kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Alisema hivi sasa anagombea udiwani katika kata ya Kiwalani hivyo mbinu zote alizokuwa akitumia akiwa upinzani atazielekeza CCM iibuke mshindi.

Alisema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa hivyo lazima juhudi zake ziweze kuungwa mkono katika kuleta maendeleo ya nchi kwani upinzani alikuwa akipoteza muda sasa hivi anakula matunda ya CCM.

Kwa upande wake mgombe ubunge wa Jimbo la Segerea, Bonah Kamoli alisema katika kata ya Minazi Mirefu na Kiwalani amefanya mambo makubwa katika kuboresha miundombinu ya kisasa ikiwemo barabara , masoko na sekta ya maji katika mradi mkubwa wa Serikali wa UMDP awamu ya kwanza ambao umepita kata hizo.

Alisema atashirikiana na wanachi wake katika kuleta maendeleo kusimamia sekta ya elimu ,sekta ya maji kwa zile kata ambazo bado hazijapata maji safi na salama pamoja na kuboresha miundo mbinu .

Naye Mgombea udiwani wa Kata Minazi Mirefu, Malisa alisema  akichaguliwa kipaumbele chake cha kwanza ni kujenga Zahanati na Shule ya Msingi ndani ya kata ya Minazi Mirefu.

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi