loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wazazi watakiwa kuwekeza katika ubunifu

WAZAZI wametakiwa kuwekeza zaidi kwenye sekta ya ubunifu kwa watoto wao ili kuwawezesha kujiajiri na kuajiri watu wengine huku wakichangia maendeleo ya jamii na nchi kwa ujumla.

Mwito huo umetolewa na Meneja wa Huduma za Kidigitali wa Benki ya CRDB, Mangire Kibanda kwenye mahafali ya 22 ya kumaliza elimu ya msingi katika shule ya Kimataifa ya Julius Kambarage Nyerere yaliyofanyika juzi shuleni hapo, jijini Dar es Salaam.

Kibanda alisema ubunifu umekuwa ni msaada mkubwa kwa maendeleo ya mataifa mengi duniani na kama ukianzishwa kuanzia ngazi za shule za msingi, sekondari na vyuo utaandaa taifa lenye maendeleo makubwa.

Alisema ili kufanikiwa kwa azma hiyo ni lazima wazazi na walezi wawekeze kwenye elimu ya ubunifu kwa watoto wao huku akiipongeza shule hiyo kwa kuliona hilo na kuanza kulifanyia kazi.

Alisema,"kama mtoto akianza kuelekezwa namna ya kuongeza thamani katika kila anachofanya au kujua namna ya kutafuta suluhu ya jambo fulani kwa njia ya kibunifu, hakika huyo akimaliza elimu yake ya msingi, sekondari na chuo anaweza kuja kuwa mtu wa muhimu kwa maendeleo ya jamii na nchi".

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Charles Bugingo alisema waliohitimu shuleni hapo ni wanafunzi 49 ambapo kati yao wa kike ni 26 na wa kiume 23.

Alisema,"tumewekeza zaidi katika sekta ya ubunifu kwa kuwa wanafunzi wanafundishwa kivitendo zaidi na kisha wanapewa nafasi ya kutosha ya kubuni mawazo mbalimbali ya kibunifu."

Pia alisema kuwa katika kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwa uhakika na kufaulu vizuri, shule imeanzisha utaratibu wa kuwapatia huduma za kulala bweni kwa wanafunzi wa darasa la nne na la saba wanaokabiliwa na mitihani ya taifa.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi