loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

TAWA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA UADILIFU

WAFANYAKAZI wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA), wametakiwa kufanya kazi kwa uadilifu katika kulinda rasilimali za nchi walizopewa kuzisimamia kwa maslahi ya taifa.

Naibu Kamishna wa uhifadhi anayeshughulikia utalii na huduma za biashara, Imani Nkuwi ametoa agizo hilo juzi wakati akizungumza na  watumishi wa  vituo  vilivyo chini ya TAWA katika mapori ya akiba ya Ugalla, Luganzo Tongwe na Wembere.

Alisema wafanyakazi kufanya kazi wa weledi na uzalendo kutasaidia TAWA kufikia malengo waliyojiwekea katika uhifadhi wa wanyamapori, misitu, mazingira na kuongeza watalii na mapato.

Nkuwi pia alitoa ufafanuzi kwa watumishi kuhusu mabadiliko mbalimbali yaliyofanywa na serikali katika taasisi za uhifadhi zilizopo nchini chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii  yenye lengo la kuboresha utalii.

"Mabadiliko yaliyofanywa ni kifungu cha 10 cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori Na. 5 ya mwaka 2009 kupitia sheria ya marekebisho mbalimbali namba 2 ya mwaka 2020,"alisema.

Alisema mabadiliko hayo yameanzisha jeshi la uhifadhi wa wanyamapori na misitu na sasa kanuni zinaendelea kuandaliwa, lakini pia sheria  imetoa baadhi ya mamlaka kwa watumishi ikiwepo kukamata wahalifu, kupeleleza na kufanya shughuli za kiintelijensia kushughulikia mashauri mbalimbali.

foto
Mwandishi: Veronica Mheta, Arusha

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi