loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Nyumba zilizotumika katika ukombozi nchini kuendelea kuboreshwa - Dk Kigwangala

WIZARA ya Maliasili na Utalii imeahidi kuendelea kuzifanyia maboresho nyumba zilizotumikiwa kama sehemu ya ukombozi na makazi ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania Baba wa Taifa  Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Kupitia mpango huo ambao tayari umeshaundiwa kamati maalumu malengo yake ni kumuenzi muasisi huyo  ambapo kupitia nyumba hizo, Serikali itaweza  kukusanya mapato  kutokana na utalii wa wageni mbalimbali watakaofika  kwa lengo la kuzitembelea.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa uzinduzi wa nyumba ya kumbukizi ya Mwalimu Nyerere iliyopo Mtaa wa Ifunda Nyumba No 63 ,Magomeni jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maliasili na Utalii Dk Hamisi Kigwangala alisema  tayari nyumba hiyo aliyokuwa akiishi Nyerere wakati wa harakati za kudai  uhuru mwaka 1950 imeingizwa katika kumbukumbu ya mambo ya kale na kuwa sehemu ya kivutio cha utalii.

Aidha Dk Kigwangala alilipongeza Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA)kwa kusimamia maboresho  ya nyumba hiyo na kuwataka kuhakikisha kuwa wanaitunza katika kipindi chote ili kulinda kumbukumbu zilizomo ndani yake humu ndani yake kukiwa na vitu mbalimbali ilivyokuwa akitumia kiongozi huyo na familia yake.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba mbali na kuipongeza Serikali kwa kukumbuka mchango wa Nyerere na kuzifanyia ukarabati nyumba alizokuwa aliishi, alisema  kiongozi huyo alikuwa mfano mzuri wa maendeleo ya taifa.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Kamishna Mkuu wa TANAPA Kijazi alisema maboresho ya nyumba hiyo yalioanza Juni mwaka jana na kukamilika Juni mwaka huu, yameifanya nyumba hiyo kuwa kielelezo tosha cha kumbukumbu ya kiongozi huyo.

 

foto
Mwandishi: Oscar Job

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi