loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Magufuli ahaidi makubwa sekta ya uvuvi

Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), John Magufuli amesema kuwa kama akipata ridhaa ya wananchi kuongoza miaka mingine mitano atahakikisha tozo mbalimbali za uvuvi zinaondolewa ili kuwapa unafuu wavuvi wadogo. 

Magufuli ameyasema hayo muda mfupi uliopita wakati akihutubia mkutano wa kampeni katika Viwanja vya Mwanakalenge-Bagamoyo mkoani Pwani.

 “Changamoto kubwa ya wavuvi wadogo ni tozo mbalimbali wanazotakiwa kutoa, mikakati ya serikali kwa miaka mitano ijayo ni kuhakikisha  inaondoa tozo zisizokuwa na tija shughuli za uvuvi zifanyike bila shida,” amesema Magufuli.

Magufuli amesema ili kuendeleza sekta ya uvuvi tayari wamelirudisha Shirika la Taifa la Uvuvi (TAFICO) na mali zake zenye thamani ya Sh bilioni 118 zilizotaifishwa na watu.

Aidha Magufuli amebainisha kuwa sheria mpya ya kusimamia uvuvi wa baharini ya mwaka 2020, imeweka mazingira rafiki kwa wanaotaka kujikita kwenye uwekezaji katika  sekta ya uvuvi kutoka nje na ndani ya nchi.

 

foto
Mwandishi: ALFRED LUKONGE

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi