loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Afrika Mashariki yaoneshwa fursa sekta ya ngozi, matunda

RIPOTI ya Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) imebainisha fursa zilizopo katika bidhaa za ngozi na mboga katika jumuiya hiyo na kuonesha nchi hizo zinapoteza mabilioni ya fedha kutoka na kuzorota kwa sekta hiyo.

Ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikiano na Taasisi ya GIZ ya ujenzi wa mnyororo wa thamani katika bidhaa zitokanazo na ngozi, matunda na mboga katika Jumuiya ya Afrika Mashariki' ilizinduliwa  Oktoba 8, mwaka huu.

Msimamizi wa Mradi EABC, Sylvester Kimeu, alisema ukanda huo una utajiri mkubwa wa rasilimali za bidhaa za ngozi ukiwa na mifugo aina ya ngombe, kondoo na mbuzi zaidi ya milioni 188.1.

Alisema licha ya mahitaji ya sasa ya ukanda huo kwa kila mwezi jozi 600,000 za viatu vya kiwandani, lakini uzalishaji ni  jozi za viatu 60,000 tu kwa mwezi.

Mkurugenzi Mtendaji wa EABC, Dk Peter Mathuki alisema sekta ya ngozi imeendelea kushuka kwa muda mrefu kutokana na uwapo mkubwa wa viatu vya mitumba  kutoka nje ya ukanda huo.

"Uagizaji wa viatu vya mitumba una gharama za chini kuliko gharama za uzalishaji kwa wazalishaji wa ndani na hivyo kupunguza soko katika sekta hiyo ambayo bado haijapata fedha za kutosha," alisema Mathuki.

Ripoti hiyo inaonesha kuna fursa kubwa ya kuongeza ukuaji wa uchumi kupitia kilimo cha bustani kwani usafirishaji wa bidhaa za mboga na matunda bado ni kwa kiasi kidogo.

“Kama ilivyoelezwa, wakulima wengi wana fedha chache kwa ajili ya kununua pembejeo huku ukosefu wa vifaa vya usindikaji karibu na vyanzo vya mazao yao pia umezuia EAC kunufaika kikamilifu na sekta hiyo.

"Miundombinu inayofaa kwa uuzaji na uhifadhi baada ya kuvuna unaweza kupunguza hasara ambazo wakulima wa bustani wanakabiliwa nazo," alisema Mathuki.

Ripoti hiyo inapendekeza serikali za nchi wanachama wa EAC kusitisha ushuru wa kuagiza na ushuru wa ongezeko la thamani kwenye mbegu na miche inayoingizwa kutoka nje pamoja na pembejeo nyingine.

Pia imependekeza kupunguzwa gharama za ushuru wa mafuta ya ndege na za  ushuru wa umeme kwa wakulima wa bustani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tasnia ya ngozi ina mchango mkubwa katika uchumi duniani  kwa makadirio ya thamani ya biashara ya takriban dola za Marekani bilioni 100 kwa mwaka, ambayo ni kubwa kuliko mnyororo wa thamani ya nyama, sukari, kahawa na chai.

"Kizuizi kikubwa kwa ukuaji wa tasnia ya viatu vya ngozi ni ukosefu wa masoko uliosababishwa na uwapo mkubwa wa viatu vilivyotumika kutoka nje pamoja na viatu vya bandia au vya plastiki ambavyo bei yake ni ya chini tofauti na  gharama kubwa za uzalishaji wa ndani."

"Ubora mdogo wa ngozi ni suala jingine lisiloweza kuepukika na ripoti imeorodhesha sababu ya pili yenye shida kwa ushindani katika minyororo ya thamani," alisema Kimeu.

Alisema kwa sasa takribani asilimia 40 ya ngozi mbichi zilizonunuliwa zinakataliwa viwandani na kasoro kubwa ni  kupunguzwa kwa kina na kutokuwa na muonekano mzuri.

WANANCHI wa Kenya wametakiwa kujiandaa kwa ongezeko la ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi