loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dodoma Queens, JKT Stars kuchuana leo

LIGI ya taifa ya mpira wa kikapu (NBL) inaendelea leo ambapo michezo minne ya wanawake na wanaume itachezwa kwenye uwanja wa Don Bosco, Dar es Salaam.

Dodoma Queens itachuana na JKT Stars wakiwa bado katika hatua ya makundi, kundi lenye timu sita.

Dodoma ni mchezo wa kwanza lakini wenzao ni wa pili baada ya kucheza wa kwanza dhidi ya Jeshi Stars na kushinda kwa vikapu 82-41.

Kila mmoja anahitaji matokeo mazuri yatakayowaweka katika nafasi nzuri ya kufuzu kwa ajili ya kutafuta washindi wawili watakaoingia hatua ya nusu fainali.

Mbali na hao, timu zingine za wanawake zitakazochuana siku tofauti ni Vijana Queens, Ukonga Queens, bingwa mkoa wa Dar es Salaam Don Bosco Lioness na JKT Stars.

Kwa upande wa wanaume watakaochuana leo ni Korogwe dhidi ya Savio, Arusha TCDC dhidi ya Oilers na Ukonga Kings dhidi ya Pazi.

Katika michezo ya awali ukiacha ya jana, Pazi imetoka kupoteza mchezo dhidi ya VBC kwa vikapu 82-63 na Ukonga Kings ikishinda dhidi ya Panthers vikapu 68-63.

Michuano hiyo inatafutwa mabingwa upande wa wanaume na wanawake watakaowakilisha nchi katika michuano ya kimataifa baadaye.

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi