loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Washauriwa kupitia orodha ya majina ya wapigakura

MSIMAMIZI wa Uchaguzi wa majimbo mawili ya Igalula na Tabora Kaskazini wilayani Uyui mkoani Tabora, Hemed Magaro amewataka wananchi kupitia orodha ya majina ya wapigakura iliyobandikwa kwenye vituo husika.

Msimamizi huyo alisema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake ambako alitoa ufafanuzi juu ya maandalizi yalivyokamilika kwa zaidi ya asilimia 85 kuelekea siku ya uchaguzi huo.

Magaro alifafanua juu kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 47 (1) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi sura 343 na kifungu 49 cha Sheria ya Uchaguzi wa Mitaa sura 292, msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Igalula na Tabora Kaskazini, wananchi wote waliojiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga kura wa rais, wabunge na madiwani mwaka huu wataruhusiwa kupiga kura kama sheria inavyoelekeza.

Msimamizi huyo alieleza kuwa vituo vyote vilivyotumika kuandikisha wapigakura ndivyo vitakavyotumika kupigia kura na vituo vya kupigia kura vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufungwa saa 10:00 jioni.

Alisema mfano wa karatasi za kupigia kura umebandikwa picha za kila mgombea na nembo ya chama chake.

Aliongeza kuwa orodha ya majina ya wapigakura kwa kila kituo cha kupigia kura imebandikwa kwenye kituo husika.

Aliwaomba wananchi wote kupitia orodha hiyo ili kutambua mapema vituo watakavyopigia kura na kuona mfano wa karatasi ya kupigia kura na mpigakura siku ya uchaguzi atatakiwa kufika kituoni na kadi yake ya mpiga kura.

Magaro alisema vifaa vyote vya kupigia kura vimewasili na kukamilika kwa asilimia 85 ambako matarajio ni vifaa vitakavyotumika ni 640.

Aidha, alitoa mwito kwa wananchi na wapigakura kwa ujumla baada ya kupiga kura warejee nyumbani na kwamba ulinzi utaimarishwa vyema na hakutakuwa na mikusanyiko isiyokuwa ya lazima.

Msimamizi huyo alimpongeza Rais John Magufuli kwa mikakati sahihi ya kusimamia nchi hasa kwa kutumia fedha za ndani kwenye uchaguzi huu na kuwaomba wananchi waiunge mkono serikali kwa kujisimamia wenyewe.

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi