loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Zungu amwombea Magufuli kura azidi kupaisha uchumi

MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Ilala kupitia CCM, Mussa Zungu amewataka wananchi wa jimbo hilo kumpigia kura Rais John Magufuli kwa ajili ya maendeleo ya sekta ya uchumi wa viwanda.

Zungu alisema hayo kwenye mkutano mkuu wa wadau wa Soko la Kimataifa la Samaki Feri, jijini Dar es Salaam.

Aliwaomba wadau na wafanya biashara wa soko hilo la samaki ifikapo Oktoba 28 mwaka huu kutofanya makosa na kumpigia kura Rais Magufuli, mgombea ubunge na udiwani kupitia CCM.

 "Wadau na wafanyabiashara wa Soko la Samaki Feri nawaomba siku ya Oktoba 28 msifanye makosa, kura zote kwa CCM mnipigie mbunge wenu na madiwani ili muweze kupata maendeleo jimboni kwetu Ilala na soko la kimataifa feri," alisema Zungu. 

Alisema Rais Magufuli katika uongozi wake amefanya mambo makubwa katika kusimamia sekta ya uchumi na viwanda ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa katika miaka mitano iliyopita wadau wa feri mumpe kura zenu kwani ni mwadilifu. 

Pia alisema Rais Magufuli ameiweka nchi sawa kwa kukemea uzembe na kumtaka kila mwananchi afanye kazi, ale kutokana na utendaji wake wa kazi.

Zungu alisema changamoto ya maji kwa sasa imeisha kwani yapo ya kutosha pia serikali imetenga Sh bilioni 1.9 kwa ajili ya ujenzi wa soko la kisasa ambapo utaanza Novemba mwaka huu.

Amewataka wadau wa Feri kushirikiana na uongozi wa soko la samaki feri kwa ajili ya maendeleo ya soko hilo.

Kwa upande wake, mgombea wa udiwani wa Kata ya Kivukoni, Sharik Choughule aliwataka wafanyabiashara na wadau wa soko la Feri wampigie kura ili aweze kuwaletea maendeleo ndani ya kata hiyo.  

Alisema kata ya Kivukoni imepata fursa kubwa ina maendeleo hivyo wananchi wakimchagua watapata maendeleo makubwa katika kuwakwamua kiuchumi.

"Mwenyekiti wetu wa Taifa John Magufuli naomba mumpigie kura amefanya mambo makubwa katika nchi yetu ya Tanzania ya Uchumi wa viwanda pamoja na mbunge wetu, Mussa Zungu na Mimi Sharik tunaomba kura zenu,"alisema Sharik.

foto
Mwandishi: Lucy Ngowi

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi