loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba, Yanga vita nafasi ya pili

 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu soka Tanzania Bara, Simba na Yanga leo wanatarajiwa kucheza katika viwanja viwili tofauti kusaka pointi tatu muhimu.

Simba itakuwa ugenini dhidi ya wenyeji Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga huku Yanga ikimkaribisha Polisi Tanzania dimba la Uhuru, Dar es Salaam.

Mechi hizo mbili ni vita ya kusaka nafasi ya pili kwa timu hizo, ambazo ziko nafasi ya pili na tatu katika mbio za kuwania ubingwa huku kila moja ikiwa na pointi 13 zikitofautiana kwa tofauto ya mabao.

Ni mchezo mgumu hasa kwa Prisons ambao wametoka kucheza dhidi ya JKT Tanzania mkoani Dodoma na kupata sare ya bao 1-1 wakiwa na uchovu baada ya kutoka safarini jana  na kisha leo wanaingia tena uwanjani kupigania matokeo.

Tofauti na wekundu hao wa Msimbazi ambao walikuwa wamepumzika muda mrefu tangu kusimama kwa timu ya taifa hawajacheza, na walipumzika kwa muda Mbeya.

Timu hizo zinakutana zikitofautiana nafasi waliyopo na ubora, Simba iko vizuri kiufundi inashika nafasi ya pili katika msimamo nyuma ya vinara Azam FC kwa pointi 13 walizopata kwenye michezo mitano ikiwa haijapoteza mchezo wowote.

Ina safu bora ya ushambuliaji yenye uchu wa kufunga muda wote ikiongozwa na Meddie Kagere ambaye huenda asiwepo leo kutokana na majeraha ila kuna anayekuja kwa kasi ya hatari Chris Mugalu amekuwa ni mwiba akifunga mabao michezo yote aliyoanza kikosi cha kwanza.

Simba iko vizuri pia, katika safu ya ulinzi ikiwa imeruhusu mabao mawili kwenye nyavu zake.

Kwa upande wa Prisons imecheza michezo sita na kati ya hiyo, imeshinda mmoja, imepata sare tatu na kupoteza michezo miwili ikiwa na pointi sita.

Matokeo yake yasiyoridhisha katika mechi zilizopita yanaifanya timu hiyo kushuka taratibu chini.

Timu hizi zinapokutana bila kujali utofauti katika ubora, mechi inakuwa ngumu kwa kila mmoja kwa sababu hukamiana. Mara 10 walizokutana kuanzia msimu wa 2015, Simba imeshinda mara sita, Prisons mara mbili na kutoka sare mara mbili.

Utakuwa ni mchezo wa presha kwa wote wawili kwa sababu, Simba imeachwa mbali na vinara Azam FC wenye pointi 21 hivyo, ni dhahiri kama inataka kutetea taji inahitaji matokeo mazuri yatakayowaweka karibu kwa maana ya kukimbizana nyuma. Na kadhalika kwa Prisons ili wasishuke zaidi chini wanahitaji kushinda.

Mchezo mwingine utakuwa wa Yanga dhidi ya Polisi Tanzania. Ni mchezo mgumu na wenye presha kila mmoja akihitaji matokeo mazuri.

Yanga inashika nafasi ya tatu nyuma ya Simba kwa pointi 13, wakiwa na uchu wa kutoka walipo na kupanda juu ikiwa na shauku ya kulipigania taji la ligi walilokosa kwa misimu mitatu.

Polisi Tanzania si timu ya kubeza wako vizuri na wamekuwa wakipanda nafasi za juu wanashika nafasi ya saba kwa pointi 11 walizopata katika michezo sita iliyopita.

Msimu uliopita Yanga ilishindwa kuchukua pointi tatu kwa Polisi, walitoka sare mechi mbili za nyumbani na ugenini.

Mchezo huo utakuwa ni mtihani wa kwanza kwa Kocha Cedrick Kaze aliyejiunga na timu hiyo hivi karibuni, wengi wakitamani kuona atakuja na mfumo gani kwani aliahidi kuleta soka la kuvutia la kushambulia na kumiliki mpira.

Yanga licha ya kuwa inafunga bado ina  ubutu katika safu ya ushambuliaji ikionekana kufunga mabao machache tofauti na wenzake walioko juu yake ila ina ukuta mzuri ikiwa imeruhusu bao moja katika nyavu zake.

Katika mchezo huo yeyote ana nafasi ya kuibuka na ushindi kutegemea na mbinu za kila mmoja.

 

 

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi