loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Azam yapania kubadili historia

VINARA wa Ligi Kuu soka Tanzania, Azam FC wamesema mara nyingi Simba na Yanga wamekuwa wakipokezana katika kuwania taji, lakini awamu hii wanataka kubadili historia.

Jeuri hiyo inakuja baada ya kushinda michezo saba ya ligi na kukaa kileleni wakiwa na pointi 21, huku wapinzani wake Simba na Yanga wakimfuata nyuma, kila mmoja akiwa na pointi 13 baada ya michezo mitano.

Akizungumza baada ya mchezo wa juzi dhidi ya Ihefu walioshinda mabao 2-0 jijini Mbeya, Kocha Msaidizi Vivier Bahati alisema wameweka malengo msimu huu watapambana kwa kila hali kuhakikisha wanachukua taji la ligi.

“Kuna timu mbili mara nyingi zimekuwa zikigombea ubingwa, lakini sisi tukasema tubadilishe stori zao, msimu huu tumedhamiria na tumejipanga kuhakikisha tunachukua taji,” alisema.

Kwa upande wa kocha wa Ihefu, Zuberi Katwila alisema kilichowaponza wakapoteza mchezo dhidi ya Azam FC ni baada ya wachezaji wake kupoteza kujiamini.

Alisema anaamini wachezaji wake watabadilika kwa vile wengi ni vijana wadogo hata akiwaingizia mbinu mpya ni rahisi kushika na kufanyia kazi.

Katwila anaanza kibarua chake kipya kwa timu hiyo baada ya kuachia ngazi Mtibwa Sugar. Timu hiyo imepoteza mechi sana wakiwa wa pili kutoka mkiani baada ya kuwa na pointi tatu tu.

Alisema anaamini kikosi hicho kitafanya vizuri michezo ijayo baada ya kufanyia marekebisho baadhi ya mapungufu yao.

 

MWISHO wa ngebe ni leo baada ya dakika ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi