loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Barcelona, Juventus, United zatakata Mabingwa wa Ulaya

ZURICH, Uswisi

BARCELONA, Juventus na Manchester United ni miongoni mwa timu zilizoibuka na ushindi katika mechi zao za kwanza za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya zilizopigwa juzi.

Lionel Messi aliweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga katika michuano 16 mfululizo ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya huku `kinda mwenye umri wa miaka 17 Pedri alifunga bao lake la kwanza wakati Barcelona ikiichapa Ferencvaros kwa mabao 5-1.

Messi alifunga bao lake kwa njia ya penalti na kuipatia Barca uongozi katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi.

Ansu Fati alifunga la pili, huku Philippe Coutinho akiongeza la tatu wakati timu hiyo ikielekea kupata ushindi huo mnono.

Gerard Pique alitolewa nje kwa kadi nyekundu, hivyo itamfanya kuukosa mchezo ujao wa ugenini  dhidi ya mabingwa wa Italia Juventus.

Juventus wenyewe waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dynamo Kyiv, huku mabao hayo yote mawili yakiwekwa kimiani na Alvaro Morata wakati kikosi cha kocha Andrea Pirlo kikianza kampeni zake za Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kwa ushindi huo.

Morata alifunga bao la kwanza baada ya pasi ya Dejan Kulusevski katika mchezo huo, ambao Juventus ilicheza bila ya nyota wao wa Ureno, Cristiano Ronaldo baada ya mchezaji huyo kukutwa na virusi vya corona.

Federico Chiesa na mchezaji aliyechukua nafasi ya Ronaldo, Kulusevski wote mashuti yao yaliokolewa na kipa Georgi Bushchan katika kipindi cha kwanza.

Mabingwa hao wa Italia pia katika mchezo huo walimkosa beki wao mzoefu, Giorgio Chiellini aliyeumia nyama za paja kabla ya mapumziko, baada ya kukaribia kufunga kwa kichwa baada ya mpira kupaa juu ya lango.

Juventus ina matumaini ya kuwa na Ronaldo, ambaye amefunga mabao 130 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya na ana medali tano za mashindano hayo, anatarajia kurejea wakati Barcelona itakapokwenda Turin katika mchezo wa raundi ijayo wa Kundi G.

Katika mchezo mwingine, Marcus Rashford alirudia maajabu yake dhidi ya Paris St-Germain baada ya kufunga bao safi la ushindi wakati Manchester United ikirejea kwa kishindo kwa ushindi wa bao 1-0.

Rashford alifunga bao hilo kwa penalti katika muda wa majeruhi na kuiwezesha United kuibuka na ushindi katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Parc des Princes.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi