loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Chelsea yamuita kipa aliyestaafu

LONDON, England

WAKATI Chelsea wakimtangaza katika kikosi chao cha Ligi Kuu mchezaji aliyestaafu Petr Cech, Arsenal wenyewe wamemuacha kiungo wao Mesut Ozil katika orodha ya wachezaji wao 25.

 Kila timu ya Ligi Kuu inatakiwa kutangaza wachezaji wake 25 wa Ligi Kuu baada ya kumalizika kwa dirisha la usajili la majira ya joto.

Cech, ambaye sasa ana umri wa miaka 38 na aliyekuwa kipa wa kutegemewa Chelsea, alistaafu kucheza soka mwishoni mwa msimu wa mwaka 2018-19, ameongezwa katika kikosi hicho kama mchezaji wa dharura.

Kwingineko, kiungo Mesut Ozil ameachwa katika kikosi cha wachezaji 25 wa Arsenal katika orodha iliyotangazwa baada ya kumalizia kwa dirisha la usajili.

Manchester United wenyewe hawajamjumuisha beki Phil Jones na kipa Sergio Romero katika orodha yao.

Beki wa kati Jones, 28, ambaye kwa mara ya mwisho aliichezea Man United wakati ikishinda mchezo wa FA Cup dhidi ya Tranmere Rovers Januari, wakati Romero mwenye umri wa miaka 33 yeye alikuwa akihusishwa na kuhamia Everton siku ya mwisho ya usajili.

Klabu zinatakiwa kutangaza kikosi cha wachezaji 25 baada ya kufungwa kwa dirisha la usajili la kimataifa na lile la nyumbani.

Cech kwa miaka 11 alikuwa akiichezea timu hiyo yenye maskani yake Stamford Bridge, huku akishinda mataji 13, yakiwemo manne ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa wa Ulaya.

Kwa mara ya mwisho kipa huyo aliichezea the Blues katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland Mei 2015, kabla hajajiunga na wapinzani wao wa London, Arsenal.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Jamhuri ya Czech baadae alirejea Chelsea katika kipindi cha majira ya joto ya mwaka 2019 akiwa na majukumu mapya akisaidia jopo la makocha wa makocha wa makipa.

"Ni kweli. Pete anafurahia mazoezi," alisema kocha wa the Blues, Frank Lampard.

"Tukiwa na Pete, ni wazi tunatarajia kitu fulani kutokea, lakini tukiwa katika matatizo hakuna yeyote bora aliye jirani yetu kuliko Petr Cech.

"Sitarajii yeye kucheza, lakini hakuna mtu anayetarajia nini kitatokea katika kipindi cha miezi sita au saba, hivyo hiyo ndio inaelezea kwanini yumo katika orodha hiyo.

Cech ni mmoja wa makipa wa nne katika kikosi cha Chelsea. Wengine ni Mhispania Kepa Arrizabalaga, kipa ghali zaidi duniani. Huku ingizo jipya Edouard Mendy akirejea juzi kutoka katika maumivu walipocheza na kutoka suluhu dhidi ya Sevilla.

Willy Caballero, 39, mara mbili aliichezea the Blues msimu huu na mara nyingi amekuwa akichaguliwa katika mashindano ya makombe hapa nyumbani.

Ozil, 32, ambaye alijiunga na Arsenal kwa rekodi ya klabu ya pauni milioni 42.4 mwaka 2013, hajaichezea the Gunners tangu Machi 7.

Mchezaji huyo wa Kijerumani, ambaye pia aliachwa katika kikosi cha timu hiyo kilichocheza Kombe la Ligi, sasa ataweza kuichezea timu ya Arsenal ya wachezaji wenye umri chini ya miaka 23 hadi pale mkataba wake utakampomalizika mwakani.

Beki wa Ugiriki, Sokratis Papastathopoulos naye pia aliondolewa.

 

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi