loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

China yatoa wito

Beijing, China

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje wa China, Zhao Lijian ametoa wito kwa nchi zote kuheshimu na kutoingilia taratibu na kanuni za nchi nyingine na zinapaswa kuunga mkono uhuru wa nchi za Africa, kulinda umoja na utulivu wao.

Alisema anaamini serikali ya Tanzania na watu wake wana hekima na uwezo wa kuandaa uchaguzi na ukafanyika kwa amani, haki na usawa.

“ Tunaamini kwamba serikali ya Tanzania na watu wake wana hekima na uwezo wa kuandaa uchaguzi, tunataka uchaguzi ufanyike kwa njia yaki, amani, usawa  na wenye mafanikio”, alisema Lijian na kuongeza kuwa kutoingiliwa katika maswala ya ndani ya nchi nyingine inapaswa kuwa kanuni ya msingi kwa nchi zote.

 

Lijian aliyasema hayo Oktoba 20 alipokuwa kwenye mkutano wake wa wakaida na waandishi wa Habari ambayo hufanya mara kwa mara.

 

Lijian alitoa maoni yake baada ya kuulizwa swali na Redio ya Kimataifa ya China(CRI) kuhusu tamko la Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania juu ya uchangazi  mkuu kuitaka serikali ya Tanzania kuunga mkono mchakato wa kidemokrasia na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua watakaoleta vurugu zinzaohusiana na uchaguzi ama kudhoofisha mchakato wa demokrasia.  

 

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi