loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Watano mbaroni Kigoma

JESHI la Polisi mkoani Kigoma imewatia mbaroni watu watano viongozi wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wilayani Kakonko wakituhumiwa kukutwa na kadi 14 za mpiga kura huku ikielezwa haijabainishwa madhumuni ya kukutwa na kadi hizo.

Kamanda wa polisi mkoa Kigoma, James Manyama alisema hayo akitoa taarifa kwa waandishi wa Habari Mjini Kigoma Jana ambapo alionya wananchi kutokubali kutoa kadi zao za kupigia kura kwa mtu yeyote.

Aliwataja waliokamatwa kuwa ni Hezron Vicent (45), Ezekia Samakere (40), Sheby Kasuka (21), Helson Miniho (38) na Denis Lubuye (30) ambao wote ni viongozi wa CHADEMA kata ya Gwanumpu.

Kamanda Manyama alisema kuwa watuhumiwa walifanyiwa mahojiano lakini hawakuwa majibu yenye mashiko kisheria kuonyesha kwanini walikuwa wanahifàdhi hizo kadi.

"Baada ya mahojiano watuhumiwa walieleza kuwa walikuwa na hizo kadi kwa ajili ya kwenda kutoa kopi kwa ajili ya kupeleka kwa Mkurugenzi wa uchaguzi wa Jimbo la Buyungu kwa ajili ya mchakato wa kuandikisha vitambulisho vya mawakala wa chama hicho Jambo ambalo kisheria halikubaliki," Alisema Kamanda Manyama.

Hata hivyo Kamanda Manyama alisema kuwa kwa mujibu wa sheria ya Taifa ya uchaguzi sura ya 343 marejeo ya mwaka 20202 kifungu Cha 90(2)  ni kosa  kisheria kwa mtu yeyote kumiliki kadi ya kupiga kura ya mtu mwingine bila kufuata taratibu.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa watuhumiwa ambao wawili hawakuwa na kadi za kupiga kura walikuwa na Nia ovu ya kuwanyima wamiliki wa kadi hizo haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka.

Akizungumzia kadi hiyo Katibu wa CHADEMA mkoa Kigoma,Shaban Madede alisema kuwa hakukuna na Nia yeyote ovu katika kadi hizo na kwamba viongozi hao walikuwa wakisaidia suala la kutoa nakala kadi hizo waweze kuziwasilisha kwa msimamizi wa uchaguzi kwa ajili ya mchakato wa vitambulisho vya mawakala.

" Kule kijijini hakuna sehemu ya kutoa nakala (Photo Copy) hivyo viongozi walikusanya hizo kadi kuja nazo Mjini wasaidie kutoa nakala na kurahisisha mchakato lakini mwisho wa siku wamekamatwa kwa madai ya kutaka kuzifanyia hujuma wakati siyo kweli," Alisema Madede.

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi