loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Magufuli afungua kiwanda cha viatu Kilimanjaro

Rais wa Tanzania Dk. John Magufuli leo amefungua kiwanda cha viatu cha Karanga kilichopo mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza kabla ya kufungua kiwanda hicho Dk. Magufuli amesema kuwa kiwanda hicho kitasaidia kupunguza tatizo la ajira na matumizi makubwa ya fedha za kigeni.

Amesema kuwa Tanzania inatumia fedha nyingi ya kigeni kuagiza viatu kutoka nje ambapo kwa mwaka wafanyabiashara huagiza jozi millioni mbili, hivyo uwepo wa kiwanda hicho utapunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya fedha hizo.

Aidha, Dk Magufuli alibainisha kuwa kiwanda hicho kitatengeneza ajira millioni tatu kwa wananchi kutoka kwa makundi tofauti wakiwemo wafugaji na mama lishe.

Kiwanda hicho kimezinduliwa kutekeleza maono ya Baba wa Taifa Julius Nyerere alipokianzisha mnamo mwaka 1978 kwa dhumuni la kutengeneza viatu vya vikosi vya ulinzi vilivyokuwa vinatekeleza opereshi kuikomboa nchi ya Uganda.

Amesema kuwa Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza 14% na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PSPF) 86% na hadi kukamilika kwake kitagharimu shilingi billioni 136.

 

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi