loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Serikali yadhamiria kumaliza ujangili

Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii, Dk. Aloyce Nzuki amesema Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inamaliza na kutokomeza masuala ya ujangiri wa wanyama pori, wizi wa mbao na uchomaji wa misitu mpaka ifikapo mwaka 2022.
 

Dk Nzuki amesema hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo ya utayari wa askari uhifadhi wa wanyama pori yalifanyika katika viwanja vya Fort Ikoma, wilayani Serengeti.
Amesema serikali imefanikiwa kupunguza ujangiri kwa asilimia 90% mpaka sasa. Dk Nzuki amesema dalili za kukomesha ujangiri ni nzuri na hadi kufikia 2020 utakuwa umekamilika.
 

Aidha, amesema kuwa licha ya mapambano yanayofanywa na serikali kutokomeza ujangiri lakini shughuli za binadamu zikiwemo uchomaji misitu, kilimo na uchimbaji zimekuwa zikiharibu rasilimali za Taifa. Dr Nzuki amesema jeshi la uhifadhi wa wanyamapori linajukumu kubwa la kuhakikisha linaendelea kulinda rasilimali za Taifa.

Kamishna wa uhifadhi wa Wakala wa misitu nchini(TFS), Profesa Dos Santos Silayo amesema hadi sasa wamefanikiwa kutoa mafunzo kwa watumishi 1264 kuhusiana na uhifadhi wa misitu na mpaka Juni mwakani maofisa 600 waliobakia watapewa mafunzo.

Amesmea mafunzo watakayotoa ni kuhusiana na udhibiti wa misitu  Nyuki na wanyama pori. Dk Silayo ameongeza kuwa wameamua kubadilisha mbinu za kupambana kwakuwa majangiri wanatumia mbinu tofauti.
Amesema shirika lao limejenga kambi mbali mbali kwenye hifadhi kwajili ya kupambana na majangiri. Mkuu wa Taasisi ya Wanyama Pori Pasiansi (PWTI), Faustine amesema waliohitimu mafunzo 302 na askari wote wanauwezo wa matumizi ya silaha. Alisema anaiomba Wizara ya maliasili kuwasaidia ujenzi wa visima katika eneo la Fort Ikoma.

 

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi