loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango azindua ujenzi viwanja vya ndege

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James amewataka viongozi wa mikoa minne ambayo inategemewa kujengwa viwanja vya ndege kuhakikisha ufuatiliaji wa karibu unafanyika kwa kila hatua pindi ujenzi wa viwanja hivyo utakapoanza.
Katibu Mkuu huyo amesema hayo hii leo kwenye uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa viwanja vinne unaotegemewa kutekelezwa katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kigoma na Rukwa.  

“Tumepata ufadhili wa Tsh. Billion 136 kutoka Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB) na ninatoa ahadi ya kutoa ushirikiano wa kutosha hadi viwanja hivi vitakapokamilika kwa mikoa husika”amesema Dotto James

Aidha, ametoa angalizo kwa wakandarasi wanaohusika na ujenzi wa viwanja hivyo kuvikamilisha kwa wakati na kama watahitaji kuongezewa muda wanapaswa kutoa sababu za msingi za kufanya hivyo.

Amesema tayari serikali imelipa fidia kwa wakazi wa maeneo ya mikoa ambayo miradi hiyo itapita ambapo Tsh. millioni 478 zimepelekwa Shinyanga, billion 3.7 Rukwa na millioni 215 kigoma.

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi