loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Nigeria ataka mazungumzo na waandamanaji

Abuja,Nigeria

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amewataka vijana wanaohusika na maandamano kusitisha mara moja  ili waweze kusogea katika meza ya mazungumzo na Serikali.

Katika hotuba yake kwa Taifa hapo jana , ikiwa ni hotuba yake ya kwanza toka maandamano hayo yaanze, amewataka waandamanaji hao wasitumike na watu wenye nia mbaya  wenye lengo la kuvuruga demokrasia ya nchi.

Hata hivyo, Buhari akugusia suala la waandamanaji kupigwa risasi na vikosi vya usalama ambapo watu wasiopungua 12 walipoteza maisha.

Maandamano hayo yalianza wiki mbili zilizopita mara baada ya kikosi cha jeshi la polisi nchini humo (SARS) kinachohusika kupambana na wizi wa kutumia silaha, ambacho kimekuwa kinashutumiwa kuwaweka watu kizuizini kinyume cha sheria na kushambulia raia kwa risasi jambo lililomshawishi Rais huyo kukivunja kikosi hicho mnamo Oktoba 11.

 

WANACHAMA wa Chama cha Republican nchini ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi