loader
Dstv Habarileo  Mobile
Ushirikiano wa Kijani: Afrika na Ulaya Pamoja

Ushirikiano wa Kijani: Afrika na Ulaya Pamoja

KATIKA kipindi cha miezi michache iliypopita, dunia yetu imebadilika kwa namna ambayo hatungeweza kutegemea mwaka mmoja uliopita. Lakini, hata kabla ya janga la COVID-19 kuikumba dunia, tulikuwa tumeshaanza kuyumba katika mwendeleo wetu kuelekea katika mustakabali endelevu.
Tulikuwa tayari tunakabiliwa na matatizo yanayohusiana na tabianchi, upotezaji wa bioanuwai na uchafuzi wa mazingira. Kulihitajika hatua kuchukuliwa ili kurudisha mwelewano kati ya dunia na uchumi, na Umoja wa Ulaya ukachukua hatua muhimu katika hilo kwa kuzindua Mpango wa Kijani wa Ulaya.

Kuanzia namna ambavyo tunazalisha bidhaa zetu hadi tunavyozitumia, Mpango wa Kijani ni mkakati wa ukuaji wenye malengo makubwa ambao unakusudia kupambana na changamoto kubwa za tabianchi na mazingira ambazo zinatukabili. Mafanikio yetu yatategemea kuungana na nchi mbalimbali tunazoshirikiana nazo kupitia ushirikiano wa kimataifa, pamoja na makubaliano ya biashara na mipango ya kimazingira. Kwa hili, tunahitaji washirika na ushirikiano.
Ushirikiano muhimu ni ule tulionao na jirani yetu wa karibu, bara pacha na mshirika wa miaka mingi: Afrika. Umoja wa Ulaya (EU) na bara la Afrika zinahitaji kuchagua mustakabali usioongeza hewa ukaa, matumizi bora ya rasilimali, na wenye kuweza kuhimili mabadiliko ya tabianchi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu. Tunaweza kufanikisha hilo kwa kuwa na ushirikiano thabiti wa kimataifa wenye malengo makubwa. Hii inamaanisha kupendekeza hatua jumuishi zinazokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na uharibifu wa mazingira, na kuzingatia masuala ya kiuchumi na kijamii.
Tunapaswa kuweka mkazo juu ya kuwa na maendeleo ya haraka katika maeneo yafuatayo yenye uwezo wa kuwa na faida kubwa kwa mabara yetu mawili: nishati endelevu na mifumo ya chakula, kulinda bioanuwai kwa kurejesha mifumo ya ikolojia, kupambana na usafirishaji haramu wa nyara za wanyamapori, na usimamizi endelevu wa misitu, ardhi na maeneo ya hifadhi. Kwa mfano, katika mradi wetu wa Eco-Boma nchini Tanzania, tumejenga mfumo wa kukabiliana na tabianchi kwa wafugaji wa jamii ya Kimasai kwa kuboresha upatakinaji wa maji kwa ajili ya mifugo, usimamizi wa nyanda za malisho, huduma za afya za mifugo, kilimo kinachostahimili ukame, nishati na elimu ya mabadiliko ya tabianchi.
Jambo moja la uhakika ni kwamba mabadiliko ya kimazingira yatahitaji uwekezaji mkubwa. Fedha za umma pekee hazitatosha. Hii ndio sababu ambayo tunashughulikia kupunguza athari za uwekezaji ili kuwezesha ushiriki mkubwa zaidi wa sekta binafsi barani Afrika na kuunga mkono maendeleo yanayozingatia mazingira kwa wote.

Wakati dunia inapambana na janga la afya, na athari zake, ushirikiano wa kimazingira kati ya Afrika na Ulaya utakuwa muhimu katika miaka ijayo. Umoja wa Ulaya (EU) utashirikiana na Tanzania na kuunga mkono juhudi zake katika kuleta maendeleo yanayozingatia mazingira ambayo huhakikisha uchumi unakuwa na mustakabali imara na wenye faida kwa wote. Kufanya kazi pamoja kwa maslahi yetu ya pamoja, Afrika na Ulaya zinaweza "kujenga tena kwa ubora" kwa kujenga dunia kijani, endelevu na jumuisha zaidi kwa wote.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/80041a231b388a46f3fad3a7eb4bde77.jpg

KWA miongo kadhaa kumekuwa na mjadala ...

foto
Mwandishi: Jutta Urpilainen, Kamishna wa Ulaya wa Ushirikiano wa Kimataifa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi