loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Fundi bomba aburuzwa kortini

FUNDI bomba na mkazi Kinondoni, Mkwajuni Juma (51) amepandishwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni kwa tuhuma za kumshambulia kwa panga Abros Vincent na kusababisha upotevu wa fedha na vitu vyenye thamani ya Sh 600,000.

Akisomewa mashitaka hayo mbele ya hakimu Hamisi Furthun, msoma mashitaka Saidi Saidi alidai kwamba mshitakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 14 mwaka huu eneo la Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.

Alidai kwamba mshitakiwa kwa makusudi, alimjeruhi mlalamikaji na kumsababishia upotevu wa Sh 200,000 taslimu na simu aina ya Galax set 3 yenye thamani ya Sh 400,000 huku akijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Mshitakiwa alikana shitaka hilo na dhamana yake ipo wazi. Alihitajika kuwa na wadhamini wawili watakaosaini ahadi ya milioni moja. Kesi hiyo itatajwa tena Novemba 3, mwaka huu.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mohamed Mussa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi