loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wahitimu darasa la 7 kufuatiliwa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Urambo mkoani Tabora imedhamiria kuwafuatilia wanafunzi waliohitimu darasa la saba.

Lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha hawatumikishwi kwenye mashamba ya tumbaku wala kuajiriwa katika ajira za aina yoyote zinazokinzana na umri wa watoto hao.

Mratibu wa Polisi Jamii Wilayani Urambo, ambaye pia anahusika na dawati wa jinsia la wanawake na watoto wilayani hapa, Yusufu John alisema hayo wakati akizungumza na wananchi na wazazi wa Kitongoji cha Mwenge Kata ya Urambo Mjini Tarafa ya Urambo.

Alisema lengo ni kuhamasisha wananchi kuacha kuwatumikisha watoto kwenye ajira hatarishi, hasa walio chini ya miaka 18.

Alisema jamii inatakiwa kuungana na kutoa taarifa, wanapoona watoto wanafanyiwa vitendo visivyofaa au wanatumikishwa

“Ninyi wananchi mnatakiwa kutuunga mkono kwa kukemea haya, watoto wenu wanatakiwa kusoma ili wawasaidie baadaye na sio kuwatumikisha hawa wanafunzi waliohitimu darasa la saba, wanatakiwa kuendelezwa na si kupelekwa kuozeshwa au kufanyishwa kazi za ndani au mashambani,”alisema John.

Ofisa Maendeleo ya Wilaya ya Urambo, Hamis Iddi alisema walipokea mtoto mwenye umri wa miaka 11 aliyeokotwa katika mnada wa ng’ombe wa wilaya. Alipelekwa na wafugaji waliopeleka ng'ombe wao mnadani hapo. Mtoto huyo alitoroka kwao baada ya kufanyishwa kazi zilizo nje na uwezo wake.

“Baada ya kumpata mtoto huyo tuliwasiliana na polisi na kutafuta utaratibu wa kumsaidia na kuwapa onyo wazazi wake endapo watarudia kitendo hicho tutawachukulia hatua kali,” alisema ofisa huyo.

Mmoja wa wananchi, Dastani Kapela kutoka Kata ya Ugala, alisema wakati huu wanafunzi wanaposubiria matokeo, wanatakiwa kupelekwa kwenye masomo ya ziada ili kujiendeleza badala ya kusalia nyumbani.

Kamati ya wilaya ya mpangokazi wa taifa wa kudhibiti ukatili kwa wanawake na watoto kwa kushirikiana na dawati la kijinsia, wameendelea kutoa elimu kuhusu hali na usawa wa watoto katika kila kata.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Lucas Raphael, Tabora

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi