loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CBT yatoa mafunzo kwa Amcos Kibaha

BODI  ya Korosho nchini (CBT) imetoa mafunzo kwa viongozi wa vyama vya msingi (AMCOS) vya zao la korosho wilayani Kibaha mkoa wa  Pwani.

Mafunzo hayo  ya siku moja kwa vyama hivyo yalihusu kilimo bora cha zao la korosho na ubora wake. Yalifanyika mjini Kibaha chini ya CBT kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo hapa nchini (TARI) Naliendele.

Lengo la mafunzo hayo ni ya udhibiti wa ubora wa korosho ghafi ngazi ya mkulima ili waweze kusimamia kikamilifu ubora wa zao hilo.

Akitoa mada katika mafunzo hayo, Mdhibiti Ubora wa Korosho kutoka CBT, Joseph Merere alisema uvunaji wa korosho ghafi, unapaswa kufanyika ikiwa imekauka juu ya mti. Kabla korosho haidondoka chini mkulima anapaswa kuhakikisha eneo la mzunguko wa matawi ya mkorosho ni safi.

Katika kuanika korosho hiyo, mkulima anatakiwa kuokota korosho angalau mara tatu kwa wiki. Kama kuna mvua ziokotwe kila siku ili kutunza ubora na zianikwe juani kwa muda wa siku tatu  hadi nne mfululizo. Zianikwe kwenye sakafu nzuri, jamvi, vitanga, mikeka au maturubai.

Mkulima anatakiwa kutenganisha korosho na uchafu mbalimbali kama vile mabaki ya mabibo makavu (kochoko), majani ya miti na vitu visivyokuwa korosho. Pia anatakiwa kuondoa korosho zilizooza, zisizokomaa, ndogo sana na zilizotoboka au kuanza kuota.

“Nasisitiza suala la umakini wa korosho, adui mkubwa wa korosho ni unyevu, kwahiyo baada ya kujiridhisha korosho imekauka vizuri tayari, ndipo iandaliwe ili kupeleka ghalani. Huko ghalani hatua ya kwanza ni kumwaga chini ili iweze kukaguliwa kisha kupakiwa kwenye gunia la katani lenye ubora uliopitishwa na TBS,”alisema Merere.

Ofisa Ushirika kutoka Ofisi ya Mrajisi Msaidizi mkoani Pwani, Eveline Macha alisema kuwa CBT imeona umuhimu wa kutoa mafunzo hayo kwa Amcos hizo na wakulima kwa ujumla. Lengo ni kuhakikisha wanafahamu kila kitu wakiwa kama viongozi wa vyama hivyo, ili wasiende kinyume na taratibu husika, kwani zao hilo linahitaji uangalifu wa hali ya juu.

Viongozi hao akiwemo mjumbe wa bodi ya Msugusugu Amcos iliyopo mjini Kibaha, Mzee Mwishehe aliiomba serikali kufikisha kwa wakati magunia katika vyama hivyo ili wahifadhi korosho mapema kabla hazijashuka viwango vinavyotakiwa.

Ally Mnola ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya Visiga Amcos iliyopo mjini humo, aliiomba serikali kuona umuhimu wa kurejesha ruzuku ya zao hilo ili kuwasaidia wakulima hao kupata pembejeo kwa wakati na kirahisi. Alisema ruzuku hiyo itawawezesha kuhudumia mashamba kwa muda mwafaka.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Kibaha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi