loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Shehe ataka viongozi wa dini kufanikisha uchaguzi mkuu

Viongozi wa Mila na Viongozi wa Dini Mkoa wa Songwe wametakiwa kutoa elimu ya uzalendo kwa waumini na wananchi ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu.

Akizungumza na viongozi wa amani katika halmashauri za Ileje, Mbozi na Tunduma, Mwenyekiti wa Amani Mkoa wa Songwe, Shehe Hussein Batuza alisema viongozi wa dini na mila, wanapaswa kukemea vitendo viovu ambavyo vinaashiria uvunjifu wa amani, ambayo imekuwa ni kivutio kwa nchi za nje.

Alisema siku chache zilizobaki ni muhimu viongozi wa dini zote, kuungana na kuepuka kutumiwa na wanasiasa kwani hali hiyo inaweza kuharibu amani

Alitaka waungane na kuipa elimu jamii kuhusu umuhimu wa uzalendo na amani kutokana na kuwa na uwezo wa kukutana na watanzania wengi ambao ni waumini wao.

“Siku hizi chache zilizobaki tuzitumie kuhubiri mambo mazuri ambayo yanahusu amani na uzalendo, lazima tushirikiane kwa pamoja kuwaelimisha waumini wetu kuhusu uzalendo… sisi viongozi wa dini tuna wafuasi wengi sana nyuma yetu ambao ndio wapiga kura na wengine wagombea. Tuna nguvu kubwa ya kukemea na kuwaambia madhara ya uvunjifu wa amani wakati wa uchaguzi,”alisema Shehe Batuza.

 

Mwenyekiti wa Machifu mkoani Songwe, Mleshelwa Nzunda alisema kuwa tayari wamewafikishia elimu wananchi kuhusu umuhimu wa kuepuka maandamano siku ya uchaguzi. Pia alisema wamewatahadharisha wananchi kuwa wasidanganywe, bali wafike kwa wingi kupiga kura na kurudi nyumbani kusubiri matokeo.

“Tayari tumewasihi wananchi wetu kuwa kazi yao ni kupiga kura tu na siyo kurundikana kwenye vituo vya kupigia kura, kwa elimu tuliyotoa tuna imani kuwa uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu ili kupata viongozi wenye uzalendo na nchi yetu,” alisema Chifu Nzunda.

Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, John Palingo aliwataka viongozi wa dini na mila, kuwaelimisha waumini wao na wananchi, kufuata taratibu na sheria zilizowekwa na serikali ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani.

Aliwashukuru viongozi wa dini kwa maombi yao, yaliyowezesha kampeni kufanyika kwa amani katika maeneo mengi nchini bila kutokea vurugu za aina yeyote.

Palingo alisisitiza kuwa ni vema viongozi wa dini watumie siku chache zilizosalia, kuhubiri amani na uzalendo ili wananchi wote watambue umuhimu wa kutunza amani na madhara ya uvunjifu wa amani. Uchaguzi mkuu utafanyika Oktoba 28, mwaka huu.

 

 

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Baraka Messa, Songwe

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi