loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viongozi wa dini wakemea wenye nia ya kuleta vurugu

VIONGOZI dini mkoani Kigoma wamewataka wagombea, viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kufuata taratibu za kukata rufaa wasiporidhika na matokeo ya uchaguzi badala ya kufanya vurugu zinazoweza kuvuruga amani na usalama wa nchi.

Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Omari Mlenda alisema hayo katika kikao cha kamati ya amani wilaya ya Kigoma na kusema kuwa kufanya fujo na kuvuruga amani siyo njia muafaka ya kuwasilisha madai malalamiko yao.

Alisema yapo maisha baada ya uchaguzi hivyo vurugu zitakazohatarisha  amani na usalama wa nchi na kufanya watu kushindwa kutekelezwa majukumu yao, zinapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Padri wa Kanisa Katoliki, Benedict Rwegoshora alitoa mwito kwa wasimamizi wa uchaguzi kuhakikisha na kuwaaminisha wadau wote wa uchaguzi kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki na atakayeshinda ndiye atakayetangazwa.

Akizungumza katika mkutano huo, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Kigoma Mjini aliwahakikishia wadau wote kwamba uchaguzi utakuwa huru na haki na atakayeshinda ndiye atakayetangazwa.

Alisema taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mgombea ubunge wa Kigoma Mjini, Kabwe Zitto kwamba kuna vituo hewa vimewekwa kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni uchochezi unaolenga kuleta vurugu na kuondoa imani ya wananchi kwa tume hiyo.

Mkuu wa Wilaya Kigoma, Samson Anga aliwatoa hofu wananchi wote kwamba uchaguzi utafanyika kwa amani na usalana na hakuna mtu atakayepata nafasi ya kuleta fujo kwani vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kulinda amani kwa mkoa mzima.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi