loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Usahihi unahitajika kabla hujatumbukiza karatasi ya kura

OKTOBA 28, 2020 iliyopangwa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani inawadia. Hata hivyo, lipo jambo ninaloona ni muhimu kukumbushana au kuelimishana.

Izingatiwe kuwa mpigakura anapopewa karatasi ya kura, akaijaza, akaikunja, bado hiyo inaitwa karatasi ya kura. Lakini akishaitumbukiza kwenye sanduku la kura, inatoka kuitwa ‘karatasi ya kura’ na kuwa ‘kura.’

Karatasi ya kura ikishatumbikizwa ndani ya sanduku la kura na kuitwa kura, hata kama mpigakura alikosea kuijaza wakati wa kuchagua anayemtaka, haiwezi kuondolewa na wala mhusika hawezi kupewa karatasi ya kura nyingine.

Katika mada kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa Sheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Athumani Kimia, anasema kulingana na  Taratibu za Upigaji Kura na Mazoezi ya Ufungaji Vituturi na Masanduku ya Kura, ikiwa kwa bahati mbaya mpigakura ameharibu karatasi ya kura, anaweza kuirejesha kwa msimamizi wa kituo.

Mfano wa kuharibu karatasi ya kura kwa bahati mbaya ni mpigakura akapiga kura bila kukusudia kwa zaidi ya mgombea mmoja, au kufanya jambo lolote linaloweza kusababisha karatasi ya kura hiyo isihesabiwe kama kura halali.

Ikiitokea hivyo, msimamizi wa kituo ataichukua karatasi ya kura iliyokosewa na kuandika nyuma yake ‘IMEFUTWA’ kisha kuiweka kwenye bahasha namba 3 A kwa uchaguzi wa rais, bahasha namba 3B kwa uchaguzi wa mbunge na bahasha namba 3C kwa uchaguzi wa madiwani. Baada ya hapo, msimamizi atampa mpigakura huyo karatasi nyingine ya kura.

Kutokana na fursa hiyo ya kidemokrasia, ikitokea mpigakura alipiga kura kwa mihemuko, lakini kabla hajatumbukiza, akakumbuka namna mgombea aliyemnyima kura alivyo mwadilifu, alivyo mchapakazi, mtumishi wa wanyonge, akaonao namna aliyemwacha alivyofanya mazuri mengi, basi mpigakura huyo asipige kura kwa masononeko, bali amwone msimamizi wa kituo na kumwomba karatasi ya kura nyingine ili apige kura makini kuchagua kiongozi bora.

Ndiyo maana ninasema hakikisha usahihi wa karatasi yako ya kupigia kura ili pia ubaini kama ina muhuri unaostahili, kabla hujaitumbukiza kwenye sanduku la kura ili iwe halali na ya kizalendo.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi