loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polisi, Mgambo, Zimamoto, Uhamiaji kusimamia uchaguzi

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro amesema majeshi yote yameunga na tayari yamesambazwa kwenye mikoa mbali mbali ikiwemo Arusha ili kusimamia uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumatano ijayo Oktoba 28.

Sirro ametaja majeshi hayo kuwa ni Polisi wenyewe, Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Mgambo ambao tayari wapo Mkoani Arusha kwa ajili ya zoezi la kuhakikisha utulivu unakuwepo siku ya kupiga kura.

Akizungumza akiwa mkoani Arusha, Sirro amesema anatambua kuwa kuna vikundi ambavyo vimepangwa kwa ajili ya kufanya vurugu siku ya uchaguzi na kuvuruga amani, hata hivyo watavikamata kabla ya siku usiku.

“Kuna vikundi vinataka  kuharibu amani katika uchaguzi jijini Arusha vitakamatwa kabla ya siku ya uchaguzi ili kuondoa malengo yao ya kuharibu  amani,”amesisitiza na kuongeza

"Arusha imekuwa na historia ya vurugu sasa tumeleta polisi wa kutosha kudhibiti wachache wanaotaka kufanya vurugu," amesema.

IGP amesema askari wanatakiwa kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unakuwa wa amani na kudhibiti changamoto zozote ambazo zitajitokeza  za kiusalama.

Hata hivyo aliwataka wananchi watoe ushirikiano wanapohisi uvunjifu wa amani ili  hatua za haraka zichukuliwe.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi