loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mtangazaji Elisha Elia kuagwa kesho, KKKT Segerea

MWANDISHI wa Habari wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Elisha Elia anaagwa kesho  saa sita mchana katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), lililopo Segerea Mwisho jijini Dar es Salaam baada ya mwili utasafirishwa kwenda Tukuyu Mbeya kwa mazishi.

Mdogo wa marehemu Ezekia Elia amesema  kaka yake huyo atazikwa katika kijiji cha Mano wilayani Tukuyu.

“Mwili wa ndugu yetu utawasili nyumbani kwa wazazi  Tabata Segerea kesho saa tatu asubuhi, baadaye utapelekwa Kanisani kwa ajili ya kuagwa,” amesema na kuongeza

“Baada ya hapo tutaanza safari ya kwenda Mbeya Tukuyu kwa mazishi. Tutazika Oktoba 27 siku ya Jumanne,” amesama na kuongeza kuwa marehemu ameacha mke na watoto wawili.

Ezekia amesema Elisha alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo na kwamba siku ya Jumanne wiki hii alipelekwa  hospitali  ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na kulazwa kwa siku nne kabla ya  kufikwa na umauti jana Jumamosi saa 10 jioni.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi