loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Messi acheza El Clasico tano bila bao

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Lionel Messi amejikuta katika wakati mgumu baada ya kucheza mechi tano dhidi ya mahasimu wao Real Madrid bila bao. Juzi Barcelona ilikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Madrid na kumfanya Messi awe na ukame wa mabao kwenye El Clasico ndani ya siku 900.

Mara ya mwisho kushuhudiwa mshambuliaji huyo kutoka Argentina akifunga bao kwenye El Clasico ilikuwa Mei 2018 katika sare ya mabao 2-2.

Messi mwenye umri wa miaka 33 amekuwa mwiba mchungu katika mechi zinazokutanisha timu hizo mbili ambapo ameshawafunga mahasimu wao hao mabao 26 kwenye mechi 41 alizocheza.

Kocha wa sasa wa Madrid Zinedine Zidane ndiye anaonekana kuwa fundi wa mbinu za kumbana Messi ambaye amewasumbua makocha wengi kila wanapowapa mbinu mabeki wao kumkaba huwa hakabiki.

Bundi alianza kumuinamia Messi katika mchezo wa Februari 6, 2019 ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kwenye mchezo huo wa nusu fainali ya kwanza ya kombe la Copa del Rey Messi alianzia benchi kitu ambacho hakikikuwa cha kawaida lakini ilibidi iwe hivyo kutokana na majeraha yaliyokuwa yakimsumbua.

Mchezo uliofuata bila Messi kufunga bao ni Machi 2, 2019 ambapo Real Madrid ilikubali kipigo cha bao 1-0 kwa bao la Ivan Rakitic.

Licha ya Messi kusumbua safu ya ulinzi lakini alijikuta mpaka mchezo unamalizika bila kufunga bao kutokana na ulinzi mkali aliowekewa na beki Dani Carvajal.

Machi mosi, 2020 ulikuwa mchezo watatu kwa Messi kutoka mikono mitu- pu ambapo Real Madrid iliibuka na ush- indi wa mabao 2-0. Kwenye mchezo huo ambao ushindi wa

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: BARCELONA, Hispania

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi