loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga utaipenda tu

KIKOSI cha Yanga chini ya kocha mpya Cedric Kaze kimeendelea kufanya vyema kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya jana kuifunga KMC mabao 2-1 kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Mbali na ushindi huo, Kocha Kaze anaonekana kudhamiria kuhakikisha timu hiyo inacheza soka la kuvutia. Yanga ikicheza uwanja wenye bahati nao ilipata matokeo yaliyoifanya kuendelea kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19.

Tuisila Kisinda aliifungia Yanga bao la kusawazisha dakika ya 41 kwa mkwaju wa penati na Wazir Junior akafunga bao la pili akiunganisha kwa kichwa kona ya Farid Mussa na bao pekee la KMC lilifungwa mapema dakika ya 26 na mshambuliaji wake Hassan Kabunda.

Huo ni ushindi wa sita mfululizo wa kikosi cha Yanga ambacho hivi sasa kipo chini ya kocha Kaze ambaye huo ni mchezo wake wa pili kuiongoza timu hiyo.

Pamoja na ushindi huo timu hiyo haikuonyesha kiwango bora kama ilivyotarajiwa huku wenyeji KMC licha ya kupoteza lakini walionekana kucheza kwa uelewano mzuri zaidi.

Katika kipindi cha kwanza KMC walifanya mashambulizi mengi kwenye lango la Yanga lakini washambuliaji wake walishindwa kuzitumia ipasavyo na kuwa faida kwa wageni wao ambao walionekana kucheza kwa mbinu zaidi huku wakitumia mashambulizi ya kushtukiza.

Kipindi cha pili Yanga walikianza kwa kasi kubwa na kusukuma mashambulizi mengi kwenye lango la KMC na dakika ya 53 kiungo Feisal Salum nusura aipatie timu yake bao la pili baada ya shuti alilopiga kugonga mwamba wa juu na mpira kurudi uwanjani kabla mabeki wa KMC kuuondoa hatari kwenye hatari.

Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu lakini dakika ya 61 Junior ‘King of CCM Kirumba’ aliiifungia timu yake bao la pili na kuwa bao lake la 60 kufunga kwenye uwanja huo akiwa na timu zote alizowahi kuzitumikia za Toto Africans na Mbao FC.

Katika mchezo huo Mwamuzi Ramadhani Kayoko aliwaonyesha kadi za njano Lamine Moro na Michael Sarpong wa Yanga kutokana na rafu ambazo walizifanya dhidi ya wachezaji wa KMC.

Matokeo mengine ya mechi za ligi jana, Mwadui FC ikiwa nyumbani uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga ilifungwa mabao 6-1 na JKT Tanzania wakati Biashara United ikishinda bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga, Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi