loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Polisi 50,000 kuajiriwa kulinda uchaguzi mkuu

JESHI la Polisi litaajiri askari maalumu 50,000 kwa ajili ya kuhakikisha uchaguzi mkuu mwakani  unafanyika kwa amani na kuzingatia sheria na taratibu.

Askari wengine 5,000 watajiunga na Jeshi la Polisi la kawaida lenye wafanyakazi 4,000 ili kufikia 100,000 kwa lengo la kuliimarisha.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Uganda, Fred Enanga alisema polisi hao maalumu watasaidia kuhakikisha sheria zinafuatwa na wataondolewa kazini baada ya uchaguzi mkuu kukamilika.

 “Tunatarajia kuajiri askari  polisi maalumu watakaofanya kazi wakati wa uchaguzi mkuu tu,” alisema.

Alisema sskari hao watalipwa  posho ya  Sh 375,200 kila mmoja kwa muda huo na kwamba wataajiriwa kutoka maeneo mbalimbali nchini mwezi mmoja kabla ya uchaguzi na mpaka kukamilika.

Alisema polisi hao watafanya kazi chini ya usimamizi wa uongozi wa wilaya na hawatapelekwa katika mafunzo maalum ya polisi.

Sifa za kuajiriwa ni kuwa raia wa Uganda, mwenye kitambulisho cha taifa, asiwe na rekodi ya matukio ya  jinai na awe na miaka 18 hadi 40 na aliyewahi kufanya kazi ya kujitolea katika jeshi la polisi.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi