loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tozo kupima corona yapunguzwa

WIZARA ya Afya imesema imepunguza tozo kwa watu wanaotaka kupima virusi vya corona katika maabara za serikali kutoka dola za Marekani 65 (sawa na Sh 240,500) mpaka dola 50 (Sh 185,000).

Hatua hiyo itahusisha pia madereva wa magari makubwa katika mipaka yote wanaotaka kufahamu hali zao za afya kwa ugonjwa huo, watu wanaotaka vyeti kwa ajili ya safari za kimataifa, taasisi zote za serikali na binafsi, wanaotaka kupima wafanyakazi wake na wageni kutoka nje ya nchi wasio na vyeti vinavyoonesha hali zao za afya.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk Diana Atwine alisema kupunguzwa kwa tozo hizo kunatokana na kupungua kwa gharama ya vifaa vya kimaabara vya kupima ugonjwa huo na vifaa vingine kutoka viwandani baada ya kuanza kwa usafiri wa anga wa kimataifa.

 

Hata hiyo, alisema serikali itaendelea kuwapima bure wagonjwa wanaopelekwa katika vituo vya afya wakiwa na dalili za ugonjwa huo, waliokutana na wagonjwa na wanaoishi katika maeneo yenye maambukizi.

Jumla ya sampuli 532, 332 zimepimwa kuanzia Machi mwaka huu baada ya kuibuka kwa ugonjwa huo.

RAIS Salva Kiir amesema serikali yake itamaliza kabisa ...

foto
Mwandishi: KAMPALA

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi