loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba mwaka wa shetani

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba  wameendelea kupoteza mchezo mbele ya timu za jeshi baada ya kuchapwa 1-0 na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hicho ni kibano cha pili kwa Simba baada ya hivi karibuni kufungwa tena 1-0 na Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

Simba imeendelea kubaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi zake 13 nyuma ya watano zao Yanga waliopo katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 19, huku Azam FC wakiongoza kwa pointi 21 baada ya kushinda menchi saba na kufungwa moja.

Katika mchezo huo wa jana, bao hilo pekee lilifungwa na Fulluzulu Maganga katika dakika ya 36 na kuiacha Simba ikipoteza mchezo huo kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Ruvu Shooting ilipata pigo baada ya mchezaji wake, Shabani Msala kutolewa kwa kadi nyekundu baada ya kumpiga ngumi Berbard Morrison katika dakika ya 74. Simba walipata penalti katika dakika ya 79, lakini John Bocco alipiga mpira uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.

Katika mchezo mwingine wa ligi hiyo, vinara wa ligi hiyo Azam FC wamejikuta wakifungwa kwa mara ya kwanza baada ya kupokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.

 Hicho ni kipigo cha kwanza kwa Azam, ambao tangu kuanza kwa ligi hiyo ilikuwa haijapoteza mchezo wowote na walitamba kuwa msimu huu ni zamu yao kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara.

Awali kabla ya mchezo huo kocha wa Azam, Aristica Cioaba alisema kuwa, kila timu imekuwa ikiipania timu yake, hivyo wana kazi kubwa kuhakikisha wanashinda.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi