loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Yanga bado sana- Kaze

KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema licha- ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) katika Uwanja wa CCM Kirumba juzi, hajaridhika na kiwango cha timu yake.

Akizungumza na gazeti hili baada ya mechi hiyo, Kaze alisema timu yake haikucheza vizuri kama alivyotarajia. 

“Ni kweli tumeshinda, lakini hatukucheza kama nilivyotarajia, KMC wenzetu walikuwa wanacheza kwa kutumia mipira mirefu muda mwingi,’’ alisema Kaze.

Alisema muunganiko wa timu yake bado sana, haswa wakati wa kudhibiti presha timu yao inaposhambuliwa.

Alisema ratiba ya ligi nayo ni ngumu kutokana na ndani ya siku 12 wanacheza mechi nne.

Kwa upande wake kocha wa KMC Habib Kondo alisema mchezo haukuwa mzuri kwa timu yake licha ya kutangulia kufunga bao huku akilalamikia penalti waliyopewa Yanga akidai haikustahili.

“Haikuwa penalti kabisa bao la kwanza la Yanga mwamuzi (Ramadhan Kayoko) alitoa penalti ili kuwarudisha Yanga mchezoni… Mchezo ulikuwa mzuri kwetu,Yanga walikuwa wanachukua mipira na kupiga tu,’’ alisema Kondo akionekana mwenye jazba.

Mshambuliaji wa Yanga SC, Waziri Junior alisema anamshukuru  kocha Kaze kwa kumpa nafasi ya kucheza.

Junior alisema ataendelea kupambana ili kuisaidia timu yake ifanye vyema katika Ligi Kuu.

Matokeo ya juzi yanaifanya Yanga kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 19 ikishinda mechi sita na sare moja katika mechi saba ilizocheza hadi sasa.

GWIJI wa muziki wa Bongo Fleva ...

foto
Mwandishi: Alexander Sanga,Mwanza

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi