loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maaskofu Katoliki wataka NEC iheshimiwe

BARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limewataka Watanzania waiheshimu na kuisikiliza Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa ndiyo mratibu wa kisheria wa uchaguzi wa Tanzania.

Aidha, maaskofu hao wamesisitiza amani na uadilifu vizingatiwe kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika kesho.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki na Amani TEC, Askofu Mkuu Jude Thaddaeus Ruwa'Ichi na Katibu Mkuu wa TEC, Padri Charles Kitima walitoa wito huo jana kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam.

Waliwataka Watanzania waongozwe na dhamiri nyoofu kwa kufanya uamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa badala ya maslahi binafsi.

Walisisitiza Watanzania kupitia imani zao wauombee Uchaguzi Mkuu uwe wa amani na salama na uzae matunda tarajiwa kwa nchi kupata viongozi bora.

Askofu Mkuu Ruwa'Ichi aliwataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kesho na kupiga kura kwa uelewa mpana, ukomavu na uzalendo na kuzingatia amani na maendeleo ya jamii.

Kiongozi huyo ambaye pia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam alivihimiza vyombo vyote vinavyohusika kuratibu na kusimamia Uchaguzi Mkuu vizingatie sheria, taratibu na maadili ya kazi ili wapigakura wawe na imani na uchaguzi huo.

"Tuwe makini kufuata sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na mamlaka husika katika kipindi hiki cha uchaguzi hususan Tume ya Taifa ya Uchaguzi." 

"Uchaguzi ni zoezi la kiraia linalohusisha haki za kirai hivyo Watanzania wote waheshimu zoezi hilo na kushiriki kwa unyofu mkubwa wa moyo, nidhamu, ukomavu, uzalendo na uwajibikaji wa hali ya juu," alisema Askofu Mkuu Ruwa'Ichi.

Padri Kitima alisema wapiga kura wanapaswa kuongozwa na dhamiri nyoofu wakati wa kupiga kura kwa manufaa mapana ya Watanzania na taifa kwa jumla.

Akiwa na Padri Chesco Msaga, Padri Kitima alisema miongoni mwa mambo muhimu yanayoweza kulivusha salama taifa katika Uchaguzi Mkuu ni vyama vyote kuwa na haki sawa.

Aidha, aliwataka wadau wa uchaguzi waheshimu matokeo yatakayotangazwa.

"Tume ndiyo refa mkuu baada mchezo anayeshinda kubali hivyo, tunaomba mratibu mkuu wa kazi hii ya uchaguzi ambaye ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi aheshimiwe  na kusikilizwa,  sisi tuna imani na tume hii hivyo wadau wake wote wazingatie uadilifu wa kisheria na kiutu kwa kuwa Mungu anataka watu wote waheshimu dhamira za watu ili tupate matokeo mazuri," alisema Padri Kitima.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi