loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Viongozi wa dini watakiwa kujieupesha na siasa

Viongozi wa dini nchini wametakiwa kuachana na mambo ya kujihusisha na siasa kutokana wengi wao wamekuwa wakisababisha uchochezi. Onyo hilo lilitolewa na  Mwenyekiti-mwenza wa kamati ya amani ya viongozi wa dini mkoa wa Mwanza,Askofu Charles Sekelwa wakati alipokuwa akizungumza na wanahabari wa mkoa wa Mwanza.

Sekelwa alisema kumekuwa na viongozi wengi wa dini wamekuwa wakitakiwa wagombea wachaguliwa kutokana na udini. Amesema kumekuwa na maneno mabaya sana yakisababisha uchochezi na kutumiwa sana na wanasiasa maneno kama ‘’ Kitanuka’’,’Tutaingia barabarani’ na ‘lazima tulinde kura zetu’.

Askofu Sekelwa aliwataka wazazi waonye vijana wao kuacha kutumika haswa katika kipindi cha uchaguzi kwa malengwa ya usababishaji wa vurugu. Aliwataka wananchi baada ya kupiga kura kuhakikisha wanaondoka na kwenda kwenye shughuli zao au kupumzika nyumbani.

Kwa upande wake sheikh mkuu wa mkoa wa Mwanza,Hassan Kabeke alisema anaiomba sana Tume ya Taifa ya uchaguzi(NEC)  kuwasaidia watu wenye uhitaji malumu kupigia kura bila kubuguziwa.

Alilipongeza Jeshi la polisi nchini kwa kulinda amani wakati wa kampeni. Aliwataka wagombea kuhakikisha wanakubali matokeo yatakapokuwa yametangazwa. Ameongeza mkoa wa Mwanza upo salama na wananchi wako tayari kwajili ya upigaji kura.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi