loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCM yajikita uchumi wa wananchi

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa miaka mitano ijayo kimejikita kuimarisha uchumi kwa wananchi katika Jimbo la Nachingwea mkaoni Lindi.

Majaliwa amesema hayo hii leo aliopokuwa akihitimisha kampeni za chama hicho kwa kumuombea kura mgombea jimbo hilo Dk. Amandus Chinguiye pamoja na madiwani.

Amesema kuwa ili uchumi uende kwa wananchi mchakato wa kufufua viwanda  vilivyokufa umeanza katika wilaya hiyo ili wakulima wawe chanzo cha kusambaza malighafi.

“Mchagueni DK Chinguiye kwakuwa ndio mtu sahihi katika ufufuaji wa viwanda vya eneo hili kwakuwa atakuwa na nafasi ya kuzungumza na rais pindi wawekezaji wanapokuja wilaya hii ipewe kipaumbele na wawekezaji hao”amesema Waziri Majaliwa.

Amefafanua kuwa chama hicho kinathamini wajasiriamali wakiwemo Baba, Mama lishe na Bodaboda kwakuwa inapozungumziwa ajira kuna ajira rasmi na zisizo rasmi ambazo mchakato unaendelea wa kuziboresha vizuri ili watanzania  waliosoma na wasiosoma kuwa na ajira.

Awali akizungumza kwa njia ya simu mgombea wa nafasi ya urais kupitia chama hicho Dk. John Magufuli amesema kuwa changamoto mbalimbali za jimbo hilo anazijua ikiwemo za zao la Korosho na ubovu wa barabara ambapo ameahadi kuzifanyiakazi.

 

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi