loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

TMA yazungumzia mvua zinazoendelea kunyesha

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema mvua zinazoendelea kunyesha katika mikoa sita nchini hivi sasa ukiwemo wa Dar es Salaam ni nyepesi.

Imesema siku mbili za mwisho wa mwezi huu mvua zinatarajiwa kuongezeka. TMA ilisema jana kuwa ongezeko hilo linalotarajiwa Ijumaa na Jumamosi kama kuna tahadhari yoyote ukiwemo uwezekano wa mafuriko wananchi wataelezwa.

Kwa mujibu wa Mchambuzi wa hali ya hewa TMA, Rose Senyagwa, mvua zinazoendelea kunyesha Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani, Unguja na Pemba si za vuli.

“Hizi mvua za sasa zinasababishwa na uwepo wa mgandamizo kidogo wa hewa katika Bahari ya Hindi na zitaendelea kwa kesho (leo) na keshokutwa (kesho) zitapungua. Lakini tarehe 30 na 31 kutakuwa na ongezeko la mvua,” alisema Senyagwa wakati akizungumza na HabariLEO.

Alisema mvua hizo zitazonyesha kwa rasharasha kwa siku tatu ni nyepesi, hazina tahadhari na kama ongezeko la Oktoba 30 na 31 litakuwa na tahadhari watawaeleza leo.

Senyagwa alikumbusha kuwa, mvua za vuli hazijaanza na akasema zitaanza wiki ya kwanza na ya pili ya Novemba kama alivyoeleza Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk Agnes Kijazi.

 

Oktoba 21 mwaka huu, Dk Kijazi alitoa taarifa kuhusu mwelekeo wa hali ya hewa kwa maeneo yanayopata mvua za msimu mara moja kwa mwaka. 

 

Dk Kijazi alitaja maeneo hayo kuwa ni mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Dodoma, Singida, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi