loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Walichosema Maalim Seif, Dk Mwinyi baada ya kupiga kura Zanzibar

Wagombea urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Hussein Mwinyi na Chama cha ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif Hamad, tayari wamepiga kura huku kila mmoja wao akiwaomba wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura.

Dk Hussein Mwinyi mara baada ya kupiga kura amesema, "Nawapongeza Wanzanzibar wote ambao wametumia haki yao ya kupiga kura na niwaombe ambao hawajafika waendelee kujitokeza kupiga kura na hatimaye zoezi liishe kwa amani", amesema Mgombea urais wa Zanziba kupitia CCM.”

Kwa upande wake Maalim Seif amesema kuwa katika Kituo cha Garagara, Jimbo la Mwera, Mjini Magharibi mambo yameenda shwari isipokuwa ana shaka na vituo vingine kwani anaamini wameweka mambo mazuri kwenye kituo hicho kwasababu yeye kiongozi anapiga kituoni hapo.

Pia amewataka wananchi waendelee kujitokeza kupiga kura kwa kuwa ni haki yao ya msingi

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Zanzibar

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi