loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Wachezaji Twiga Stars, U-17 waahidi makubwa

WACHEZAJI wa timu za wanawake za soka za Tanzania, wamesema wako tayari kwenda kushindana na kurudi na kombe katika mashindano ya Cosafa yanayotarajiwa kufanyika Afrika Kusini kuanzia Novemba 3-14.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, nahodha wa timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 17 na ile ya Twiga Stars walisema kama ambavyo timu ya U-20 ilivyofanya vizuri mwaka jana na wao wanakwenda kurudi na Kombe.

Nahodha wa U-17, Noela Luhalu alisema wanakwenda Afrika Kusini kwa lengo moja tu la kurudi na kombe na si vinginevyo.

“Makocha wametuandaa vema na TFF imetulea vizuri hivyo tunawaomba Watanzania watuombee maana lengo letu ni kurudi na kombe,” alisema Noela.

Naye nahodha wa Twiga Stars, Amina Bilal alisema wanajua wamealikwa katika mashindano hayo kwa sababu wana timu bora, hivyo watakwenda kuonesha ubora wao kwa kutwaa ubingwa.

Twiga Stars imepangwa Kundi C na itafungua dimba kwa kucheza na Zimbabwe, Novemba 4 katika Uwanja wa Wolfson na U-17 itacheza na Comorro siku hiyo hiyo.

Naye Kocha Mkuu wa timu hizo, Bakari Shime alisema wachezaji wako tayari kwa mashindano na anachofanya ni kuendelea kufanya marekebisho ya makosa yanayojitokeza katika mazoezi na kuwajenga kisaikolojia.

“Kwa asilimia kubwa vikosi vyote ambavyo viko kambini vimeimarika na wako tayari na mashindano na nina imani watakwenda kushindana ili warudi na kombe,” alisema Shime.

Timu za Twiga Stars na U-17 zimealikwa kushiriki mashindano ya Cosafa yanayotarajiwa kuanza Novemba 3-14 na ya U-17 yataanza Novemba 5-14 na timu zinatakiwa kuripoti Oktoba 31.

Mwaka jana ilialikwa timu ya U-20 na ilichukua ubingwa wa mashindano hayo.

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Rahel Pallangyo

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi