loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Kale Amboni Cave Marathon yaja

KALE Amboni Cave Marathon inatarajia kufanyika Februari 7, mwakani jijini Tanga, imeelezwa.

Akizungumza na gazeti hili kutoka Tanga mwandaaji wa mbio hizo, Sophia Murra alisema jana kuwa mbio hiyo itakuwa ya aina yake na lengo kubwa likiwa ni kuhamasisha utalii wa ndani.

Mbali na hilo pia mbio hiyo itasaidia kuinua uchumi wa wafanyabiashara wa Tanga na mkoa kwa ujumla, kwani itashirikisha wakimbiaji wengi ambao watakula, kulala na kutembelea mapango ya Amboni.

Murra alisema kuwa pia mbio hiyo itasaidia kuibua na kukuza vipaji vya wanariadha chipukizi ambao wamejaa mkoani Tanga, lakini wameshindwa kutoka kwa sababu mbalimbali, lakini kupitia mbio hiyo wataibuliwa na kuendelezwa.

Alisema kuwa tayari ameshapata vibali vyote kutoka Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) na sehemu zingine zote ili kufanikisha mbio hiyo, ambayo itashirikisha nusu marathoni, kilometa 10, tano na 2.5 kwa watoto wadogo.

Akizungumzia udhamini, Murra ambaye ni mkimbiaji wa mbio nyingi alisema kuwa milango iko wazi kwa wote wanaotaka kudhamini mbio hiyo, ambayo inatarajia kuandaliwa kwa kufuata taratibu zote zinazokubalika na Riadha ya Dunia (WA).

MWANAMITINDO wa Marekani Halima ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi