loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba yaanza kumeguka

BENCHI la ufundi la klabu ya Simba limeanza kumeguka baada ya meneja Patrick Rweyemamu na kocha wa makipa Muharami Mohammed kufukuzwa kazi kutokana na timu hiyo kupoteza michezo miwili mfululizo.

Simba ilipoteza dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 kwenye  uwanja wake wa nyumbani wa Uhuru, Dar es Salaam na dhidi ya Tanzania Prisons kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga na kuanza kuibua maneno kuwa huenda kuna jambo ndani ya timu hiyo.

Akizungumza jana, Rweyemamu alikiri kuachana na mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Ni kweli nimeachana nao na nitakuwa nje ya mpira kwa sasa acha nipumzike kidogo,” alisema Rweyemamu.

Hata hivyo habari za ndani zilieleza kuwa, kocha, Sven Vandebroeck alikuwa haelewani na meneja huyo lakini baadaye alikuja kufahamu kuwa wanagombanishwa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.

“Kocha ameshangaa kusikia Rweyemamu amefukuzwa. Kweli mwanzo walikuwa hawaelewani lakini kocha alikuja kujua wanagombanishwa na kuweka mambo sawa na walikuwa hawana tatizo tena,” kilisema chanzo.

Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting kocha Sven alitoa kauli iliyotafsiriwa kama ni fumbo na inawezekana kukawa kuna kitu kinaendelea ndani ya timu hiyo.

 “Sifikiri kama tumefungwa kwa sababu ya ‘game fitness’, ni ngumu kwa wakati huu kutaja ni nini tatizo hususani kama utaeleza kila kitu katika vyombo vya habari,” alisema Sven.

Kufukuzwa kwa Rweyemamu na Muharamu kutokana na vikao vya ndani vilivyofanyika juzi kuwekana sawa, kwani hata ndani ya uongozi inadaiwa hali si shwari na inasemekana timu amesusiwa Salim Abdallah ‘Try Again’ na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez.

Habari za ndani zinadai mmoja wa viongozi ambaye yupo karibu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya klabu, Mohamed Dewji ‘Mo’ haelewani na viongozi wenzake na amekuwa akimfanyia majungu mmoja wa viongozi waandamizi wa Friends of Simba na aliyewahi kuwa kiongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Mwingine aliyefukuzwa kazi ni mwandishi wa tovuti ya klabu hiyo, Ally Shatry ‘Chico’ na habari za ndani zinasema klabu imedai haiwezi kumudu gharama za kumlipa.

Katika msimamo Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 13, huku Azam FC ikiongoza ikiwa na pointi 21 ikifuatiwa na Yanga yenye pointi 19 na Biashara inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 16.

KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi