loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Morrison kukosa pambano dhidi ya Yanga

KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison ataukosa michezo mitatu ikiwemo mchezo wa watani wa jadi dhidi ya Yanga unaotarajiwa kupigwa Novemba 07, 2020.

Sambamba na adhabu hiyo, pia atatakiwa kulipa faini ya Sh 500,000 ikiwa ni sehemu ya adhabu iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyoketi Oktoba 27, 2020 kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na TFF mapema leo, Morrison ataanza kutumikia adhabu hiyo kwa kukosa mchezo dhidi ya Mwadui FC na ule wa Kagera Sugar.      

Wengine waliopata adhabu kama ya Morisson ni mabeki Juma Nyosso (Ruvu Shooting) na Salum Kimenya (Prisons).

Katika hatua nyingine, kamati hiyo pia imemfungia kwa mwaka mmoja mwamuzi Shomari Lawi kutojihusisha na mchezo wa soka kwa kosa la kutomudu mchezo pale ambapo Prisons ilipocheza na Simba katika Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga.

 

KOCHA wa Yanga, Cedric Kaze amewashusha ...

foto
Mwandishi: Alfred Lukonge

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi