loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Mambosasa: Wanaotishia kuingia barabarani, mkono wa sheria unawangoja

KAMANDA wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amewaonya wanaotoa vitisho vya kuingia barabarani kuwa watakutana na mkono wa sheria na kutaka watanzania kuwapuuza kwani suala hili halina afya kwa nchi.

Kamanda huyo ameonya kuwa kipindi cha kampeni kimeisha na sasa wapo kazini kuhakikisha sheria za nchi hazichezewi na mtu yeyote.

Akizungumza baada ya kutembelea Kituo cha kuhesabu kura cha Jimbo la Ilala ambalo ndilo litakalotumika kutangaza matokeo ya ubunge kwa majimbo ya Ilala ,Segerea na Ukonga amesema kwa sasa hali iko shwari na watu wanaendelea na majukumu yao kama kawaida.

"Uchaguzi ni kushindanisha wagombea kwa sera na jinsi walivyojiuza. Matokeo ya nani atashinda ni maamuzi ya wananchi baada ya kupiga kura jana. Nawataka wananchi kuwa wavumilivu wakati zoezi la kuhesabu kura likiendelea, iwapo kuna ambao watalazimisha kuandamana barabarani basi watakukuta mkono wa sheria unawasubiri,"amesema Mambosasa

Aidha amebainisha kuwa katika suala la usalama hataki lichezewe na mtu yeyote kwani yupo kuwalinda wanaochukia vurugu na fujo ili wabaki salama.

Rais wa Tanzania Dk John Magufuli ...

foto
Mwandishi: Theopista Nsanzugwanko

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi