loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Shehe ataka maombi kumaliza tofauti za kisiasa

SHEHE Bashart Rehman Butt wa Jumuiya ya Kiislamu ya Ahmadiyya amewaomba viongozi wa madhehebu ya dini mbalimbali nchini, kuwahimiza waumini wao kuwaombea wagombea wa vyama vya siasa watakaochaguliwa ili wafanye kazi kwa kushirikiana.

Ametaka maombi hayo yaambatane na wagombea kuwawezesha kuondoa tofauti zao za kiitikadi za vyama vyao vya siasa, ili kila mmoja awajibike kuliletea taifa maendeleo.

Kiongozi huyo wa dini alisema hayo kwenye Maadhimisho ya Sherehe ya Maulid alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa. 

Bashart alisema maombi hayo ni muhimu kwa viongozi watakaochaguliwa ili kuondoa tofauti zao zilizokuwapo katika kipindi cha harakati za uchaguzi hususan wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita.

Mintarafu Sikukuu ya Maulid, aliwaomba waumini wa dini ya Kiislamu kusherehekea sikukuu hiyo  kwa kukumbuka jamii ya watu wasiojiweza na walio katika mazingira magumu.

Alisema moja ya mafundisho ya Mtume Muhammad (S.A.W) ni pamoja na kuwakumbuka watu wasiojiweza, hivyo akawaomba waumini wenye uwezo kuwakumbuka watu hao katika kipindi chote.

Aidha, aliwataka waumini kuwakumbuka wagonjwa wakiwamo walio  hospitalini, wafungwa na watu wenye ulemavu wasiojiweza kimaisha.

Kwa mujibu wa Shehe Bashart Rehman Butt, waumini wa Kiislamu wanapaswa kujiepusha na chuki na dharau kwa jamii inayowazunguka.

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi