loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Prof. Jay: Si ni kweli ninakubalika Jamani…..Siyo Mzee!!

WANANCHI  tupo pamoja hapo?  Siyo mzee

Watanzania tunaelewana kule ?  Siyo Mzee

Washika Dau na Wapiga Debe hapo?   Siyo Mzee

Eeeh?  Siyo Mzee

Eti?  Siyo Mzee

Hicho ni kibwagizo cha Wimbo wa Profesa Jay katika wimbo wake wa  Siyo Mzee/ Kikao cha Dharura,  ambao unalenga wanasiasa ambao wanarudi kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuwaongoza tena, na ndivyo unavyoweza kusema kuwa Wananchi wa Mikumi wamemkataa baada ya kuangukia pua kwenye kura za Ubunge Jimbo la Mikumi.

Jay ambaye alikuwa anatetea jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka mitano kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Jimbo hilo limemponyoka baada ya mpizani wake  Denis Londo  wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuibuka kidedea.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Mikumi amemtangaza Denis Londo  wa CCM kuwa mshindi wa nafasi ya kiti cha Ubunge kwa kupata kura 31,411 sawa na asilimia 62.7 dhidi ya mpinzani wake Joseph Haule ‘Prof Jay’ wa CHADEMA aliyepata kura 17,357 sawa na asilimia 34.7

Prof Jay ameliongoza Jimbo la Mikumi kwa kipindi cha miaka mitano baada ya kushinda kwenye Uchaguzi uliopita mwaka 2015.
 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi