loader
Dstv Habarileo  Mobile
TPA
Picha

Waajiri watakiwa kuchangia mabadiliko mifumo ya ajira

WAAJIRI wametakiwa kuchangia mabadiliko katika mifumo ya ajira kwa taasisi za elimu ya juu ili kupata wahitimu watakaokidhi vigezo katika ajira kwa umahiri wautakao.

Hayo yalisemwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) anayeshughulikia taaluma, Profesa Deus Ngaruko wakati wa warsha ya kufunga Mradi wa EPICA ambao chuo hicho kilishiriki kama mdau katika kuandaa mifumo ya kutathimini maendeleo ya mwanafunzi pamoja na uwepo wa mwajiri.

Alisema waajiri ndio wanaohusika katika uendeshaji wa shughuli za kila siku, hivyo wana nafasi kushauri vyuo vikuu katika uandaaji wa mitaala ambayo itasaidia kupata wahitimu watakaokuwa na sifa za soko la ajira.

Alisema iwapo vyuo vikuu vinafundisha kwa mifumo ya wakati uliopita ili kuwapa maarifa wanafunzi wa sasa wanapaswa kujitathimini kwa kuwa kuna maarifa mapya katika kila dakika kumi na mbili.

Vyuo vikuu vina aina ya utekelezaji unaotakiwa kufuatwa kwa mujibu wa sheria na taratibu za mamlaka za udhibiti ambao unaweza kuchangia kutofanyika kwa utekelezaji wenye tija kwa muda muafaka,alisema.

Mratibu wa mradi huo OUT, Dk Edefonce Nfuka alisema matokeo ya mradi huo yamethibitisha kupatikana kwa suluhu ya changamoto katika masuala ya uajiri kwa kuwa unahusisha mwanafunzi, mwajiri na taasisi ya elimu katika kipindi chote cha mwanafunzi kujifunza.

Mratibu wa Ufundishaji na Kujifunza OUT, aliyeshiriki kama Mratibu wa Mbinu za Ufundishaji katika mradi huo, Dk Lawi Yohana alisema mradi huo unakwenda sambamba na sera ya elimu ya taifa ya mwaka 2014 ambayo inalenga kuandaa wahitimu wenye umahiri kwenye maeneo ya kazi.

Alisema mfumo huo unaenda sambamba na mipango ya nchi hususani sera ya viwanda ambapo utasaidia wahitimu kuwa mahiri katika ubunifu na uundaji wa zana na mashine ndogondogo zitakazotumika katika usindikaji na kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa nchini.

foto
Mwandishi: Vincent Mpepo, OUT

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi